IQNA

UN: Facebook imehusika na uchochezi dhidi ya Waislamu wa Rohingya

15:58 - March 13, 2018
Habari ID: 3471427
TEHRAN (IQNA)- Wachunguzi wa Umoja wa Mataifa wameulaumu mtandao maarufu wa kijamii wa Facebook kuwa umehusika kwa uchochezi wa mauaji ya umati dhidi ya Waislamu wa jamii ya Rohingya nchini Myanmar.

Kwa mujibu wa Marzuki Darsuman, mwenyekiti wa Kamati Huru ya Kimataifa ya Umoja wa Mataifa ya Kutafuta Ukweli Kuhusu Myanmar, amesema mitandao ya kijamii imekuwa na nafasi kubwa katika kuchochea mauaji ya kimbari dhidi ya Waislamu.

Amesema maandishi na taswira za kuchochea mauaji ya Waislamu wa Myanmar zimekuwa zikisambazwa kupitia Facebook pasina mtandao huo wa kijamii kuchukua hatua kuzuia au kufuta propaganda hizo za kichochezi.

Mkaguzi wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia faili la Myanmar Yanghee Lee amesema Facebook ina nafasi muhimu katika masiha ya umma na binafsi nchni Myanmar na serikali ya nchi hiyo hutumia mtandao huo wa kijamii kueneza taarifa kwa umma. Amesema badala ya Facebook kuleta pamoja jamii nchini Myanmar imetumika kamaa chombo chakuchochea maangamizi ya umati ya Waislamu.

Kuanzia Agosti  25 mwaka huu hadi sasa vikosi vya usalama vya Myanmar vimechoma moto vijiji visivyopungua 350 katika eneo la Waislamu huko Rakhine magharibi mwa nchi hiyo.

Jinai kubwa wanazofanyiwa Waislamu hao na wanajeshi na Mabudha wa nchi hiyo  wenye misimamo ya kufurutu katika mkoa wa Rakhine magharibi mwa Myanmar zilishika kasi tangu tarehe 25 mwezi Agosti mwaka huu. Hadii sasa  jina hizo zimepelekea kuuliwa Waislamu zaidi ya elfu sita na kujeruhiwa maelfu ya wengine huku wengine karibu laki saba wakilazimika kuwa wakimbizi katika nchi jirani ya Bangladesh.

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa uhalifu unaofanywa na Mabudha kwa himaya ya serikali nchini Myanmar dhidi ya Waislamu wa jamii ya Rohingya ni mauaji ya kimbari.

Zeid Ra'ad Al Hussein anasisitiza kwamba, kuna udharura wa kufika katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo na kufanya uchunguzi kuhusu ukatili unaofanywa na serikali ya Myanmar dhidi ya Waislamu.

3465388

captcha