IQNA

Mkuu wa OIC, Papa Francis Wasisitiza Mazungumzo Baina ya Dini

21:40 - March 17, 2018
1
Habari ID: 3471431
TEHRAN (IQNA)-Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu, OIC, Yousef bin Ahmad al-Othaimeen amekutana na Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis na kumshukuru kwa msimamo wake kuhusu Waislamu Warohingya na suala la uhamiaji.

Katika taarifa , OIC imesema al-Othaimeen na Papa Francis wamekutana Ijumaa mjini Vatican ambapo walisisitiza kuhusu mazungumzo baina  dini huku wakisisitiza kuhusu hekima na kuishi kwa maelewnao ili kukabiliana na misimamo mikali na ugaidi.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, al-Othaimeen amemsisitizia Papa Francis kuwa ugaidi hauna nafasi yoyote katika dini na kwamba OIC inalaani vitendo vyote vya kigaidi kutoka katika dini yoyote.

"Al Othaimeen pia amemshukuru Papa Francis kutokana na msimamo wake kuhusu Quds Tukufu (Jerusalem) na haki za Waislamu na Wakristo katika mji huo mtakatifu."

Aidha Katibu Mkuu wa OIC pia amempongeza papa kwa msimamo wake wa kuunga mkono Waislamu Warohingya wanaokandamizwa Myanmar na wahamiaji.

3465409

Imechapishwa: 1
Inatathminiwa: 0
Haiwezi kuchapishwa: 0
Bila jina
0
0
Hongera
captcha