IQNA

Rais wa Iran awatumia Waislamu salamu za Idi

20:43 - June 15, 2018
Habari ID: 3471559
TEHRAN (IQNA)- Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewatumia mkono wa Idi viongozi wa nchi za Kiislamu na Waislamu wote kwa mnasaba wa sikukuu ya Idul Fitr.

Katika ujumbe wake, Rais Hassan Rouhani amesema: "Kwa baraka za sikukuu iliyojaa baraka na rehema na chini ya kivuli cha kutii amri za Mwenyezi Mungu ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, ni matarajio yangu kuwa umma wote wa Kiislamu utakuwa umepata unyofu na usafi wa nyoyo na matendo katika mwezi huu na kila mmoja wetu atajitahidi kadiri inavyowezekana kujiidilisha kubakia katika njia tukufu ya kufikia kwenye ukamilifu wake wa kibinadamu."

Rais Rouhani aidha amesisitiza kuwa, ni matumaini yangu umma wa Kiislamu utaweza kutumia vizuri mafundisho ya kijamii yanayopatikana katika sikukuu hii azizi na tutaweza kushuhudia mshikamano na mfungamano zaidi wa Waislamu katika kupambana na machafuko na misimamo ya kuchupa mipaka. Ni matumaini yangu tutaweza kuitumia vizuri sikukuu hii kuleta umoja na wahda baina ya Waislamu katika kukabiliana na siasa za mabeberu wa dunia wasio na mwamana na wanaojikumbizia kila kitu upande wao, kama ambavyo ni matarajio yangu umoja na mshikamano huo wa Waislamu utaweza kuleta amani na utulivu katika kona zote za dunia.

Katika sehemu ya mwisho ya ujumbe wake huo, Dk Rouhani amemuomba Mwenyezi Mungu Mtukukfu kulinda heshima na ufanisi wa Waislamu wote duniani.

Sehemu kubwa ya nchi za Kiislamu duniani zimesherehekea sikukuu ya Idul Fitr ya mwaka huu wa 1439 Hijria, leo Ijumaa Juni 15, 2018 ambayo imesadifiana na mossi Shawwal.

3722896

captcha