IQNA

Qarii wa Iran ashinda mashindano makubwa zaidi ya Qur’ani ya Televisheni

11:36 - June 16, 2018
Habari ID: 3471561
TEHRAN (IQNA)- Qarii wa Qur’ani kutoka Iran, Ustadh Ali Asghar Shoaei, ameibuka mshindi katika duru ya 11 ya Mashindano ya Qur’ani ya mubashara kupitia Televisheni ya Kimataifa ya Al Kawthar.

Kwa mujibu wa Idara ya Mahusiano ya Umma ya Al Kawthar, Ustadh Shoae amepata pointi 84 kati ya 100 katika fainali ya mashindano hayo.

Nafasi ya pili imechukuliwa na Ustadh Fathullah Bibres wa Misri ambapo alipata pointi 82.5 huku Mohammad Taqi Anvari wa Afghanistan akishika nafasi ya tati kwa kupata pointi 81. Washiriki kutoka Lebanon na Iraq wameshika nafasi za nne na tano kwa taratibu.

Mashindano ya 11 ya Kimataifa ya Qur’ani ya إِنَّ لِلْمُتَّقِينَ مَفَازًا , "Hakika wachamngu wanastahiki kufuzu"  yalianza katika siku ya kwanza ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kuendelea hadi siku ya mwisho ya mwezi huo mtukufu.  Katika mashindano hayo ya qiraa au kusoma Qur’ani yanyaofanyika kwa mwaka wa 11 sasa, washiriki kutoka kila kona ya dunia walishiriki moja kwa moja (live au mubashara) kwa njia ya simu. Katika mashindano ya mwaka huu mbali na kupiga simu, pia washiriki waliweza kushiriki kwa njia ya taswira kupitia mtandao wa Skype. Halikadhalika mwaka huu washiriki waliweza kutumia njia ya intaneti kuona pointi walizopata wakati mashindano yakiendelea.

Majaji wa mashindano ya mwaka walitoka nchi kadhaa za Kiislamu kama vile Misri, Syria, Iraq na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Mashindano hayo ya Qur’ani mubashara kupitia televisheni yametangtazwa kuwa makubwa zaidi ya aina yake duniani.

3722934

captcha