IQNA

Wanasesere waliovishwa Hijabu, "Madada wa Salam"

17:30 - June 18, 2018
Habari ID: 3471564
TEHRAN (IQNA)- Hivi karibuni nchini Uingereza kumeanza kuuzwa wanaserere waliovishwa Hijabu maarufu kama "Salam Sisters" au "Madada wa Salam" ambao ni nembo ya mwanamke Muislamu anayeweza kuigwa.

Wategenezaji wa wanaserere  hao waliovishwa hijabu wanasema wamewategeneza kwa kuzingatia watu kutoka tamaduni, kaumu na rangi mbali mbali duniani kwa lengo la kuwafunza wasichana Waislamu kuwa wanaweza kufanikiwa wakiwa wamevaa Hijabu. Aidha wanaserere hao waliovishwa Hijabu wanakusudia pia kutoa mafunzo wa wasichana kutoka dini na rangi zote kutizama tafauti zao kwa mtazamo chanya na kwamba tafauti baina ya wanadamu kutoka  dini, kaumu au rangi tafauti ni nukta ya nguvu.

Wanaserere hao wamebuniwa na mtengeneza mitindo Mwislamu kutoka Australia, Peter Gould, ambaye anasema alitaka mabinti zake wawe na wanaserere wanaowakilisha hali halisi ya maisha yao.  Shirika la Zileej, linalosimamiwa na Gould, ndilo ambalo limeunda wanaserere hao waliovishwa Hijabu kamili.

 

Wanasesere waliovishwa  Hijabu,

 

Wanasesere waliovishwa  Hijabu,

 

Wanasesere waliovishwa  Hijabu,

3723429

captcha