IQNA

Polisi Uganda wapata mafunzo kuhusu sheria za Kiislamu

22:07 - November 19, 2017
Habari ID: 3471270
TEHRAN (IQNA)-Polisi nchini Uganda wamepata mafunzo kuhusu sheria za familia na watoto katika dini tukufu ya Kiislamu.

Mfunzo hayo ambaye yametolewa kwa kitengo maalumu cha polisi wanaohusika na masuala ya familia yameandaliwa kwa hisani ya Mwambata wa Utamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Kampala kwa ushirikiano wa Ofisi ya Mufti Mkuu wa Uganda menye makao yake katika Msikiti wa Kibuli.

Katika warsha hiyo ya siku moja iliyojumuisha maafisa 70 wa polisi katika ukumbi wa mikutano wa Msikiti wa Kibuli, washiriki walipata mafunzo kuhusu maudhui mbali kama vile, familia, ndoa na talaka kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu. Aidha walipata mafunzo kuhusu namna ya kukabiliana na hitilafu za kifamilia kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu.

Akizungumza katika warsha hiyo, Mwambata wa Utamaduni wa Iran mjini Kampala Bw. Ali Bakhtiari ameelezea matumani yake kuwa maafisa wa polisi katika kitengo cha familia wataweza kutekeleza majukumu yao wakiwa na ufahamu sahihi kuhusu Uislamu na waweze kuchangia kutatua hitilafu za kifamilia zinapoibuka.

Aidha ametahadharisha kuhusu kuhujumiwa familia na itikadi za kidini kufuatia kujipenyeza mila na desturi za kimagharibi na kusema hicho ni chanzo kikuu katika kuvurugika familia.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mufti Sheikh Suleman Kasule alisema Uislamu ni dini ya mahaba na urafiki na kwamba talaka haihimizwi hata kidogo isipokuwa tu wakati hakuna budi tena.Polisi Uganda wapata mafunzo kuhusu sheria za Kiislamu

Polisi ya Uganda imemshukuru mwambata wa utamaduni wa Iran mjini Kampala kwa kuandaa warsha hiyo ambayo imetajwa kuwa ni yenye manufaa kwa maafisa walioshiriki.

3664672

captcha