IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Kupiga marufuku mazungumzo na Wamarekani kutawazuia kujipenyeza nchini Iran

17:32 - November 03, 2019
Habari ID: 3472199
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema mazungumzo na Marekani hayajakuwa na matokeo yoyote na kusisitiza kuwa: " "Kupiga marufuku mazungumzo na Marekani ni moja ya njia muhimu za kuwazuia kujipenyeza nchini Iran."

Ayatullah Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameyasema hayo leo katika mkesha wa Tarehe 13 Aban (Novemba 4) ambayo ni "Siku ya Kitaifa ya Kupambana na Ubeberu na Uistikbari wa Kimataifa." Ayatullah Khamenei amebaini kuwa, kuzuia njia ya kujipenyeza tena kisiasa na kuwa na satwa Wamarekani nchini Iran ni jibu muhimu zaidi la Jamhuri ya Kiislamu mbele ya njama za watawala wa Washington.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema mazungumzo na Marekani hayajakuwa na matokeo yoyote na kusisitiza kuwa: "Mazungumzo na Marekani hayajakuwa na faida kwa sababu hawataki kulegeza msimamo hata kidogo."

Akihutubu hapa Tehran mbele ya hadhara kubwa ya maelefu ya wanafunzi kutoka kote Iran kwa mnasaba wa siku hii, Kiongozi Muadhamu ameongeza kuwa: "Upande wa pili katika meza ya mazungumzo unatazama kushiriki wakuu wa Iran katika mazungumzo kuwa na maana ya kuipigisha magoti Jamhuri ya Kiislamu ya Iran." Amebaini kuwa sisistizo lao la kutaka mazungumzo ni kwa lengo la kuwafahamisha walimwengu kuwa 'mashinikizo ya juu zaidi' na vikwazo vimefanikiwa na Wairani wamepigishwa magoti.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema uzoefu kuhusu mazungmzo ambayo hayakuwa na natija ya Marekani na Cuba na pia Marekani na Korea Kaskazini ni somo kubwa na kuongeza kuwa viongozi wa Marekani na Korea Kaskazini walikutana lakini hatimaye, Wamarekani kama ilivyo kawaida yao katika mazungumzo,  hawakuondoa  vikwazo hata kidogo na wala hawakulegeza msimamo hata chembe."

Kiongozi Muadhamu aidha ameashiria sisitizo la serikali ya Ufaransa kuwa mpatanisi na kusema: "Rais wa Ufaransa anasema mkutano na Trump utapelekea kutatuliwa matatizo yote ya Iran. Tunapasa kusema huyu bwana ima ni mjinga na haelewi au yuko pamoja na Wamarekani."

Ayatullah Khamenei ameendelea kwa kuhoji, je, matakwa ya Marekani kwa Iran yatafikia kikomo wapi, na kuongeza kuwa: "Matakwa ya Marekani kamwe hayana kikomo."

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria jitihada zisizo na natija za Marekani kwa lengo la kuweka vizingiti au kufuta kabisa uwezo wa Iran katika sekta ya makombora ya kujihami na kusema: "Leo, kwa uwezo Wake Mwenyezi Mungu na hima ya vijana wetu, tuna makombora yenye uwezo wa kulenga kwa ustadi umbali wa maelfu ya kilomita."

3854207

captcha