IQNA

Safari ya Hija ya mtu tajiri zaidi katika historia

19:39 - August 04, 2020
Habari ID: 3473031
TEHRAN (IQNA) –Kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu, ibada ya Hija ni wajibu kwa kila Mwislamu mwenye uwezo wa kifedha na kiafya.

Wakati mtu tajiri katika historia alipoelekea katika safari ya Hija karne kadhaa zilizopita, nini kilichojiri?

Mansa Kankan Musa alikuwa Mfalme wa 10 wa Ufalme wa Mali, anatajwa kuwa mwanadamu tajiri zaidi katika historia.

Alitawala Mali baina ya miaka 1312 hadi 1337 Miladia na alikuwa mfalme wakati Ufalme wa Mali ulipokuwa katika kilele cha adhama yake.

Kwa mujibu wa jarida la Time, Mansa Musa ni kati ya watu matajiri zaidi katika historia. Weledi wa historia wanasema iwapo utajiri wa Mansa Musa utahesabiwa kwa thamani ya sasa, basi alikuwa na utajiri wenye thamani ya takribani dola bilioni 400 uliotokana na uchimbaji dhahabu katika Ufalme wa Mali.

Mansa Musa, ambaye alijitahidi sana kustawisha Uislamu katika nchi yake, aliweka historia kutokana na safari yake ya Hija.

Mnamo mwaka 1324, Mansa Musa aliamua kufunga safari kuelekea Hija, Safari hiyo ilifanyika kuanzia mwaka 1324 hadi 1325. Kwa mujibu wa riwaya za historia, msafara wa Hija wa Mansa Musa ulikuwa na watu 60,000 na wote walikuwa wamevaa mavazi yaliyoshonwa kwa hariri ya Kiirani iliyokuwa maarufu sana wakati huo. Msafara wake ulikuwa na maelfu ya ngamia na ndovu 100.

Aidha msafara huo ulikuwa na watumishi 12,000 ambapo kila mmoja alikuwa amebeba kilo 1.8 ya dhahabu. Mansa Musa alihakikisha kuwa kila mtu na mnyama aliyekuwa katika msafara wake alipataka chakula na mahitaji yote. Msafara huo ulikuwa na ngamia maalumu 80 ambapo kila ngamia alikuwa amebeba kilo 23 hadi 136 za dhahabu. Mansa Musa alikuwa mtu karimu na hivyo alimpa zawadi ya dhahabu kila masikini aliyekumbana na msafara wake. Katika kila mji aliopita,ikiwemo miji ya Cairo na Madina, alipeana zawadi za dhahabu. Baadhi ya riwaya zinasema kuwa kila Ijumaa katika safari yake alikuwa akijenga msikiti. Safari ya Mansa Musa ilikuwa ikiandikwa na waandishi wataalamu katika msafara wake. Inadokweza kuwa Julai mwaka 1224 alikutana na mfalme wa Misri wa wakati huo, Nassr Muhammad.

Kutokana na ukarimu mkubwa wa Mansa Musa, bei ya dhahabu ilianguka na kusababisha hasara ya $1.5bn katika uchumi wa eneo la Asia Magharibi (Mashariki ya Kati).Safari ya Hija ya mtu tajiri zaidi katika historia

Inaarifiwa kuwa, alipokuwa akirudi nyumbani, Mansa Musa alpitia tena Misri akajaribu kusaidia uchumi wa taifa hilo kwa kuondoa dhahabu iliokuwepo kupitia kuiomba kwa bei ya juu kutoka kwa wafanyibiashara wa Misri.

Ukarimu wa Mansa Musa ulimpa ummarufu yeye na ufalme wake wa Mali kote dunaini.

Mansa Musa alirejea Mali kutoka Makka akiwa ameandamana na wanazuoni wa Kiislamu, wakiwemo Masharifu, ambao ni kutoka kizazi cha Mtume Muhammad SAW.

Ni wakati huo ndio mji wa Timbuktu uliopimarika na kuwa kituo cha elimu ambapo watu walisafiri kutoka maeneo mbali mbali duniani ili kusoma katika kile ambacho baadaye kiliitwa Chuo kikuu cha Sankore.

3914399/

captcha