IQNA

Sheikh Raed Salah atahadahrisha kuhusu njama za Israel dhidi ya Msikiti wa Al Aqsa

15:15 - August 10, 2020
Habari ID: 3473052
TEHRAN (IQNA) – Mwanaharakati maarufu wa kupigania ukombozi wa Palestina ametahadharisha kuhusu njama za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Msikiti wa Al Aqsa ulio katika mji wa Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu na utawala huo.

Sheikh Salah ambaye ni mwenyekiti wa Harakati ya Kiislamu katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu yaani Israel, ameshiriki katika warsha iliyoandliwa na Kamisheni ya Quds Tukufu ya Jukwalii la Kiraia la Ankara (ACSP) la Uturuku kabla ya kuanza kutumikia kifungo cha miezi 28 gerezani kuanzia Agosti 16.

Amesema utawala wa Israel ulianza njama zake kwa kuukalia kwa mabavu mji wa Quds mwaka 1967na kwamba tokea wakati huo Israel imekuwa ikitekeleza njama mbali mbali dhidi ya Msikiti wa Al Aqsa.

Amesema vyama vyote vya kisiasa katika utawala wa Kizayuni wa Israel zinaafikiana kuhusu kuendelea kuudhibiti mji wa Quds na kuuharibifu Msikiti wa Al Aqsa.

Mpango wa Muamala wa Karne uliopendekezwa na Marekani mwezi Januari unajumuisha kukabidhiwa kikamilifu Israel mji mtakatifu wa Quds wenye Kibla cha Kwanza cha Waislamu yaani Msikiti wa al Aqsa, vitongoji vilivyoko katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan vyote ipewe Israel, Wapalestina wasiwe na haki ya kurejea kwenye ardhi za mababu zao na makundi ya muqawama wa Palestina yapokonywe silaha ili kusiwe na jambo lolote linalohatarisha usalama wa utawala wa Kizayuni wa Israel.

3472232

captcha