IQNA

Afisa wa Umoja wa Mataifa

Facebook imekataa kuwasilisha ushahidi wa jinai dhidi ya Waislamu wa Myanmar

18:13 - August 11, 2020
Habari ID: 3473058
TEHRAN (IQNA) – Mkuu wa taasisi ya Umoja wa Mataifa inayochunguza jinai dhidi ya Waislamu wa jamii ya Rohingya nchini Myanmar amesema Shirika la Facebook limekataa kutoa ushahidi wa jinai za kimataifa hata baada ya kuahidi kushirikiana kuhusu katika kadhia hiyo.

Nicholas Koumjian, mkuu wa taasisi ya Umoja wa Mataifa ya Uchunguzi Huru  Kuhusu Myanmar (IIMM) ameliambia Shirika la Habari la Reuters kuwa, shirika hilo kubwa la mtandao wa kijamii wa Facebook linashikilia ushahidi ambao ni muhimu sana katika kuchunguza jinai zilizotendekea Myanmar lakini hadi sasa limekataa kukabidhi  ushahidi huo.

Koumijian hakutana aina ya ushahidi unaoshikiliwa na Facbook. Shirika la Facebook nalo hadi sasa halijatoa taarifa kuhusu kadhia hiyo.

Serikali ya Manymar imefikishwa aktika Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu kutokana na oparesheni ya kijeshi yam waka 2017 ambayo ilipelekea Waislamu zaidi ya 730,000 kutoka jimbo la Rakhine kukimbilia katika nchi jirani ya Bangladesh. Myanmar inakanusha kuwa wanajeshi wake walihusika katika mauaji ya kimbari huku ikidai kuwa wanajeshi walikuwa wakitekeleza oparesheni dhidi ya wanamgambo.

Wachunguzi wa Umoja wa Mataifa wanasema mtandao wa kijamii wa Facebook ulitumika kueneza hisia cha chuki dhidi ya Waislamu na hivyo kuchochea mauaji ya kimbari. Shirika la Facebook linasema linajitahidi kuzuia uenezwaji fikra za chuki katika mtandao wake wa kijamii na kwamba limefuta akaunti zinazohusishwa na jeshi la Myanmar lakini limehifadhi data au taarifa za chuki zilizkuwa zimesambazwa.

Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa lilianzisha taasisi ya  Uchunguzi Huru  Kuhusu Myanmar (IIMM)  mwaka 2018 ili kukusanya ushahidi kuhusu jinai za kimataifa zilizotendwa Myanmar kwa lengo la kutumia ushahidi huo katika kesi zitakazofunguliwa siku za usoni.

Wiki iliyopita, Facebook ilipinga ombi la Gambia la kutafa taarifa ziliozokuwa zimetumwa katika mtandao huo na maafisa wa kijeshi na polisi nchini Myanmar. Gambia imewasilisha kesi ya mauaji ya kimbari dhidi ya Myanmar katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai, (ICJ), yenye makao yake The Hague Uholanzi.

Facebook ilitoa taarifa na kusema haiwezi tekeleza ombo la Gambia lakini ikaahidi kushirikiana na IIMM.

3472254

captcha