IQNA

Wasioamini wanapoelekea kwa Mwenyezi Mungu

15:58 - May 19, 2022
Habari ID: 3475264
TEHRAN (IQNA) – Wakati fulani mwanadamu hukumbana na hali ngumu ambazo hakuna mtu anayeweza kumuelewa wala kumsaidia na hivyo huelekea kuomba msaada kwa yule mwenye nguvu ambaye anajua yuko karibu.

Hata wasioamini wanaokana kuwako kwa Mungu wanaweza nyakati fulani kutafuta msaada kutoka kwa Mungu.

Wakati fulani Mungu huwaweka watu katika hali kama hiyo ili kuwapa muhula wa kufikiria tena na kutafakari maisha yao ili wabadili njia yao.

Aya za 22 na 23 za Surah Yunus zimeashiria hali hiyo ifuatavyo:

Yeye ndiye anaye kuendesheni bara na baharini. Hata mnapo kuwa majahazini na yakawa yanakwenda nao kwa upepo mzuri wakaufurahia, upepo mkali ukawazukia, na yakawajia mawimbi kutoka kila upande, na wakaona wamesha zongwa, basi hapo humwomba Mwenyezi Mungu kwa kumsafishia niya: Ukituokoa na haya bila ya shaka tutakuwa miongoni mwa wanao shukuru. (22)

Lakini akisha waokoa, mara wanafanya jeuri tena katika nchi bila ya haki. Enyi watu! Jeuri zenu zitakudhuruni wenyewe. Hii ni starehe ya maisha ya dunia tu. Kisha marejeo yenu ni kwetu, na hapo tutakuambieni mliyo kuwa mkiyatenda. (23)

Katika Tafsiri yake ya Nuru (Noor) ya Qur'ani Tukufu, Hujjatul Islam Muhsin Qara’ati anaangazia baadhi ya jumbe za aya hizi mbili:

1- Sheria zinazotawala katika maumbile ziko chini ya amri Yake Allah: ...“Yeye ndiye anaye kufikisha kwa nchi kavu na baharini...”

2- Anachofanya mwanadamu pia kinaweza kuhusishwa na Mungu, kwa sababu nguvu halisi ni yake. Ingawa mwanadamu anasafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine, Mwenyezi Mungu anasema: "...Yeye ndiye anayekuendesha nchi kavu na baharini...."

3- Haijalishi ni maendeleo kiasi gani mwanadamu anafanya, bado anaweza kukumbwa na kwa majanga ya kimaumbe na maafa: “…upepo mkali na mawimbi huja juu yao kutoka kila upande...”

4- Wale ambao wana mambo ya kidunia na ustawi wa dunia wasifikiri kwamba hali itabaki hivyo daima: Hata mnapo kuwa majahazini na yakawa yanakwenda nao kwa upepo mzuri wakaufurahia, upepo mkali ukawazukia, na wakaona wamesha zongwa

5- Maafa ya kimaumbile na matatizo yanamfanya mwanadamu afikirie upya tabia yake na kuacha kiburi: “…basi hapo humwomba Mwenyezi Mungu...

6- Wakati mwanadamu anapokuwa kwenye hatari, Fitra (maumbile asili) yake humfanya awe ni mwenye kuelekea na kumzingatia zaidi Mwenyezi Mungu: ..."basi hapo humwomba Mwenyezi Mungu kwa kumsafishia niya."

7- Imani na Ikhlas (nia takasifu) lazima ziwe za kudumu na sio za muda tu na wakati wa hatari: ..."wakaona wamesha zongwa, basi hapo humwomba Mwenyezi Mungu kwa kumsafishia niya..."

8 -  Mwanadamu anaahidi wakati wa hatari, lakini anapofikia ustawi, anapuuza,..." Ukituokoa na haya..."

9 -  Kutokushukuru na kukufuru baraka ni miongoni mwa misingi ya dhiki na adhabu. "Lau ungelituokoa na haya, tusingelishukuru: lau ungelituokoa, bila shaka tungeshukuru. Lakini akisha waokoa, mara wanafanya jeuri tena katika nchi bila ya haki. Enyi watu! Jeuri zenu zitakudhuruni wenyewe."

* "Tafsir Noor" ni kitabu chenye juzuu 12 kilichoandikwa na Hujjatul Islam Mohsen Qaraati ambaye ni mwanazuoni na mfasiri wa Qur'ani Tukufu kutoka Iran aliyezaliwa mwaka wa 1959 huko Kashan. Tafsiri yake imeandikwa kwa lugha sahali kufahamika na maelezo yake ni mafupi kwa kuzingatia kikamilifu aya za Qur'ani Tukufu

captcha