IQNA

Hasira Uingereza baada ya wanafunzi Waislamu kulishwa nyama ya nguruwe

16:45 - May 19, 2022
Habari ID: 3475266
TEHRAN (IQNA)- Shule moja nchini Uingereza imewalisha wanafunzi Waislamu nyama ya nguruwe jambo ambalo limeibua hasira kali miongoni mwa wazazi.

Kwa mujibu wa taarifa,  Shule ya Msingi ya Ryders Green ya West Bromwich mjini Birmingham Jumatano imewalisha wanafunzi Waislamu soseji za nyama ya nguruwe badala ya soseji za mboga. Wakuu wa shule wanadai wanafunzi hao wamelishwa soseji ya nguruwe kimakosa.

Uzembe huu wa shule umepelekea wazazi wa watoto Waislamu wakasirike sana na kuanzisha malalamiko dhidi ya kitendo hicho kinachoonyesha kutojali hisia za Waislamu.

Msemaji wa shule amesema kosa halikufanywa na shule bali ni kosa la kampuni ambayo imepewa kandarasi ya kupika chakula na kwamba imetakiwa itoe maelezo.

"Tunalichukulia swali hili kwa uzito na tayari tumeshawasilisha malalmiko kwa shirika lenye kupika na pia kwa Mamlaka ya Viwango vya Chakula.

3478959

captcha