IQNA

Ibada ya Hija

Muislamu wa Uingereza awasili Makka baada ya kusafiri kwa miezi 10 kwa Miguu

15:52 - June 29, 2022
Habari ID: 3475441
TEHRAN (IQNA) – Muislamu Muingereza mwenye asili ya Iraq aliwasili Makka siku ya Jumapili baada ya kuanza safari ya miguu zaidi ya miezi 10 iliyopita nchini Uingereza.

Adam Mohamed, 52, alikuwa ameanza safari kwa miguu mnamo Agosti 1, 2021, akilenga kuwasili Saudi Arabia kabla ya kuanza kwa Ibada ya Hija ya mwaka huu.

Mohamed alipitia nchi kadhaa zikiwemo Ujerumani, Bulgaria, Uturuki, Syria na Jordan, akitembea karibu kilomita 6,500.

"Siku moja niliamka tu na nikasema nitatembea kuelekea kuelekea Makka kwa ajili ya Hija, ndivyo nilivyofanya, na njiani nilimuom,ba Mwenyezi Mungu aturehemu na atusamehe sisi wanadamu, sote. Sisi sote, sio tu kabila moja, au kaumi mmoja, au imani moja, kila mtu,” Mohamed aliwaambia waandishi habari mwishoni mwa Agosti 2021.

Akisukuma mkokoteni wenye uzito wa hadi kilo 250 na ukiwa na vipaza sauti vya mawaidha ya Kiislamu, Mohamed alisema anaeneza ujumbe wa upendo, amani na usawa.

Wakati alipowasilia Makka Jumapili 26 Juni, alilakiwa na waumini wa msikiti unaojulikana kama Masjid Aisha. Amesema katika muda wote wa safari yake, amekuwa akilakiwa na kukirimiwa na watu mbali mbali.

Saudi Arabia ilitangaza mwaka huu kwamba itawaruhusu Waislamu milioni moja - kutoka ndani na nje ya ufalme huo - kutekeleza ibada ya Hija ikilinganishwa na takriban 60,000 mwaka jana na chini ya 1,000 mnamo 2020.

Moja ya nguzo za Uislamu, Hija ni wajibu kwa Waislamu wote ambao wana uwezo angalau mara moja katika maisha yao.

4067334

captcha