IQNA

Umoja na Amani

Chuo Kikuu cha Al Mustafa kinahimiza umoja, mazungumzo

19:40 - July 02, 2022
Habari ID: 3475452
TEHRAN (IQNA) – Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa amesema chuo hicho kinajikita katika kukurubisha madehebu za Kiislamu, umoja, mazungumzo na maelewano baina ya dini.

Hujjatul Islam wal Muslimin Ali Abbasi ameyasema hayo katika mkutano na balozi mpya wa Iran nchini Lebanon, Mujtaba Amani, na kuongeza kuwa ni kwa sababu hii ndio chuo hicho kinawakubali wanafunzi kutoka madhehebu mbali mbali za Kiislamu n ahata dini nyinginezo.

Akiashiria harakati za chuo hicho nchini Lebanon amesema Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa kina nafasi muhimu katika kutoa mafunzo kwa nguvu kazi ya sekta ya utamaduni na elimu nchini humo.

Amesema matawi mawili ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa nchini Lebanon hutoa shahada za uzamili na uzamivu kwa watafiti Walebanoni.

Amani, kwa upande wake, amepongeza shughuli za kielimu na kiutamaduni za Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa katika nchi mbali mbali huku akielezea matumaini kuwa ushirikiano na chuo hicho unaweza kufungua uga mpya katika diplomasia ya umma ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa (SAW) ni chuo cha Kiislamu ambacho kilianzishwa kwa lengo la kuarifisha Uislamu kwa dunia kupitia mbinu na teknolojia za kisasa.

4068088

captcha