IQNA

Jinai za Israel

Hamas yapongeza ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu mzingiro wa Wazayuni Gaza

19:57 - July 03, 2022
Habari ID: 3475456
TEHRAN (IQNA) - Harakati ya Mapambano ya Kiislamu wa Palestina Hamas imepongeza ripoti ya Ofisi ya Masuala ya Haki za Binadamu (UNOCHA) ambayo ilionyesha kuhusu madhara ya mzingiro wa utawala haramu wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza..

"Ripoti hii inachukuliwa kuwa hati mpya ya Umoja wa Mataifa iliyoongezwa kwa msururu wa ripoti za zamani ambazo zinafuatilia uhalifu na ukiukwaji unaotendwa na Wazayuni," msemaji wa Hamas Abdel-Latif al-Qanou alisema katika taarifa.

Al-Qanou alitaka jamii ya kimataifa kuuwajibisha utawala wa Kizayuni wa Israel kutokana na "ukandamizaji na uchokozi" dhidi ya Wapalestina.

Pia alitaka jamii ya kimataifa kushinikiza  Israeli kukomesha ukiukwaji wake na mashambulio dhidi ya Wapalestina, na pia kuondoa mzingiro dhidi ya  Gaza.

Ripoti ya UNOCHA imebaini kwamba mzingiro wa  bahari, anga na nchi kavu unaotekelezwa na Israel dhidi ya ukanda wa Gaza"imezidisha hali mbaya, kutokana na kuzuia bidhaa ndani na nje kupitia njia zinazodhibitiwa na Israeli."

Aidha ripoti hiyo inasema, "Viwango vya ukosefu wa ajira huko Gaza ni kati ya kiwango cha juu zaidi ulimwenguni: kiwango cha ukosefu wa ajira cha robo ya kwanza 2022 kilikuwa asilimia 46.6, ikilinganishwa na wastani wa asilimia 34.8 mwaka 2006.

"Asilimia 31 ya kaya huko Gaza zina shida kukidhi mahitaji muhimu ya elimu kama ada ya masomo na vitabu, kwa sababu ya ukosefu wa rasilimali za kifedha, na Wapalestina milioni 1.3 kati ya milioni 2.1 huko Gaza (asilimia 62) wanahitaji msaada wa chakula," ripoti hiyo imeongezwa.

Tangu mwaka 2006 utawala wa Kizayuni wa Israel umeliweka eneo la Ukanda wa Gaza chini ya mzingiro wa pande zote. Sababu kuu ya mzingiro wa utawala wa Kizayuni dhidi ya watu wa Gaza ni ushindi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) katika uchaguzi wa Bunge la Palestina na kushindwa harakati ya Fat'h, na vilevile makubaliano ya kiusalama kati ya Misri na utawala wa Kizayuni. Ijapokuwa serikali iliyotokana na uchaguzi huo wa Bunge la Palestina ilisambaratika kutokana na mizozo ya ndani, na harakati ya Fat'h ikachukua tena madaraka, lakini mzingiro wa utawala wa Israel haujaisha na unaendelea hadi hii leo licha ya kupita miaka 15 sasa. 

Kutokana na mzingiro huo, Gaza imekumbwa na maafa makubwa. Kuzingirwa kwa miaka 15 eneo la Gaza kumesababisha uhaba wa chakula katika eneo hilo kiasi kwamba, Umoja wa Mataifa na Shirika la Chakula na Kilimo la umoja huo (FAO) pia wameeleza wasiwasi wao kuhusu suala hilo. Kwa mujibu wa ripoti ya Kituo cha Utafiti wa Masuala ya Kisiasa na Kiuchumi cha Palestina, mwaka 2021 zaidi ya nusu ya familia za Wapalestina hazikuwa na usalama wa chakula.

3479551

Habari zinazohusiana
captcha