IQNA

Jinai za Israel

Kanisa la Presbyterian Marekani latangaza Israel kuwa utawala wa kibaguzi

20:30 - July 03, 2022
Habari ID: 3475457
TEHRAN (IQNA)- Kamati ya Kanisa la Presbyterian nchini Marekani imepitisha azimio la kutangaza Israeli utawala wa ubaguzi au apathaidi.

Azimio hilo limepitishwa Jumanne lilikuwa moja ya sera kadhaa zinazohusiana Asia Magharibi au Mashariki ya Kati iliyochukuliwa na Kamati ya Ushirikiano ya Kimataifa ya baraza kuu la kanisa hilo wakati wa mkutano mkuu wa madhehebu ya Waprotestanti huko Louisville, Kentucky.

Azimio hilo ambalo limeungwa mkono wa wanachama 28 na kupingwa na wanachama watatu, limesema limetambua kwamba sheria, sera, na mazoea ya Israeli yanajumuisha ubaguzi dhidi ya watu wa Palestina.

Aidha azimio hilo limebaini kuwa vitendo vya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya watu wa Palestina "hutimiza ufafanuzi wa kisheria wa kimataifa wa ubaguzi wa rangi au apathaidi.

Halikadhalika azimio  hilo linalinganisha sera za Israeli katika Ukingo wa Magharibi na yale yaliyokuwa yakijiri wakati wa utawala wa ubaguzi wa rangi au apathaidi huko Afrika Kusini wakati "kulikuwa na ukosefu wa haki, mateso yaliyoenea, na ukandamizaji mkubwa wa haki za binadamu.”

Mapema Juni pia huko Manchester, NH, jimboni New Hampshire Marekani, Kongamano la New England la Makanisa ya Methodist ilipitisha kwa wingi azimio lenye kichwa “Kutambua na Kupinga Ubaguzi wa Rangi Katika Ardhi Takatifu.”

Azimio hilo lilitanguliwa na matamshi kadhaa kuhusu hali halisi ya maisha ya Wapalestina katika Ardhi Takatifu na kubainisha kuwa, mashirika kadhaa ya kutetea haki za binadamu yametoa ripoti zinazobainisha mfumo wa utawala wa Israel ni wa kibaguzi, ikiwemo B. 'Tselem mwaka 2021, Human Rights Watch mwaka 2021, na Amnesty International mwaka 2022.

4068246

captcha