IQNA

Mshauri wa Rais wa Iran

Kuna haja ya kuwafahamisha vijana kuhusu utambulisho wa kijinai wa Marekani

7:10 - July 04, 2022
Habari ID: 3475459
TEHRAN (IQNA)- Mshauri wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika masuala ya kaumu na waliowachache kidini amesema kuna haja ya kuwafahaisha vijana utambulisho halisi wa Marekani ambayo inatenda jinai lakini inadai kutetea haki za binadamu.

Mamusta Abdulsalam Karimi Mshauri  wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika masuala ya kaumu na waliowachache kidini ameyasema hayo Jumapili katika 'Kongamano la Nne la Kimataifa Kuhusu Haki za Binadamu za Kimarekani Kwa Mtazamo wa Kiongozi Muadhamu' na kusema: "Marekani inadai kutetea haki za binadamu katika hali ambayo yenywe ni mkiukaji wa haki za binadamu na hivyo ni wajibu kwa wote kufichua uso mchafu na khabithi wa watawala wa Marekani."

Aidha amesema kundi la kigaidi la ISIS au Daesh limetokana na fikra za Kimarekani.

Mshauri wa Rais wa Iran ameendelea kusema kuwa, Marekani inadai kutetea haki za binadamu lakini hakuna chochote kinachoonekana katika nchi hiyo isipokuwa ukiukwaji wa haki za binadamu. 

Kwingineko katika kauli yake, amesema lengo la kuundwa serikali za mitume wote ni kuleta uadilifu wa kijamii.

Katika kalenda ya Iran tarehe 27 Juni hadi tatu Julai hutambuliwa kama Wiki ya Haki za Binadamu za Kimarekani ambapo katika wiki hii utambulisho halisi wa jinai za Marekani hubainishwa wazi mbele ya walimwengu na hivyo kufichua hadaa ya Marekani katika madai yake kuwa eti ni mtetezi wa haki za binadamu. Katika wiki hii pia huangaziwa zaidi jinai za Marekani dhidi ya Wairani wasio na hatia.

Moja ya jinai za Marekani dhidi ya watu wa Iran ilijiri miaka 34 iliyopita ambapo ndege ya abiria aina ya Airbus ya shirika la ndege la Iran iliyokuwa ikitoka Bandar Abbas, kusini mwa Iran kuelekea Dubai, ilishambuliwa kwa makombora mawili ya jeshi la Marekani kwenye maji ya Ghuba ya Uajemi. 

4068371

captcha