Kiongozi mwandamizi wa Baraza la Uhusiano wa Kiislamu nchini Marekani (CAIR) ameitaka Polisi ya Marekani FBI kuacha kufanya ujasusi ndani ya Misikiti nchini humo.
2014 Nov 15 , 20:33
Ban Ki-moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametangaza kuwa, kumeundwa kamati ya uchunguzi kuhusiana na jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel katika ukanda wa Gaza.
2014 Nov 13 , 09:57
Makundi ya kutetea haki za binadamu yamearifu kuwa, Waislamu wa jamii ya Rohingya wamelazimishwa kuondoka nchini Myanmar katika wiki 3 ziliopita kutokana mpango mpya wa serikali uliozusha mjadala.
2014 Nov 09 , 21:38
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amemteua Dakta Muhammad Sarafraz kuwa Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB) kwa kipindi cha miaka mitano.
2014 Nov 08 , 20:59
Sheikh Ahmad Karima Mhadhiri mwandamizi katika Chuo Kikuu cha al Azhar nchini Misri amepigwa marufuku kufundisha na siku zijazo atafunguliwa mashtaka mahakamani, kwa kosa eti la kuitembelea Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
2014 Nov 04 , 19:23
Waislamu wa Kishia nchini Misri wamemwalika Sheikh Mkuu wa al-Azhar kuhudhuria shughuli ya maombolezo ya Ashura ya kukumbuka kuuawa shahidi Imam Hussein mjukuu wa Mtume Muhammad SAW.
2014 Oct 31 , 16:02
Ayatullah Hashemi Rafsanjani, Mkuu wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amemwandikia barua Mfalme Abdullah bin Abdulaziz wa Saudi Arabia ya kumtaka azuie kutekelezwa hukumu ya adhabu ya kifo iliyotolewa dhidi ya mwanazuoni wa Kishia wa nchi hiyo Sheikh Nimr Baqir an-Nimr.
2014 Oct 26 , 07:14
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei ametuma salamu za rambi rambi kufuatia kuaga dunia Ayatullah Mohammad-Reza Mahdavi Kani, Mkuu wa Baraza la Wanazuoni Wataalamu Wanaomchagua Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.
2014 Oct 21 , 19:58
Spika wa Bunge la Italia amesema kuwa, dini ya Kiislamu haipaswi kufungamanishwa na vitendo vya kufurutu mipaka vinavyofanywa na makundi ya kitakfiri na kigaidi kama vile Daesh na kusisitiza kwamba jamii ya kimataifa inapaswa kuelewa kwamba misingi ya dini ya Kiislamu ni kutangaza amani na upendo na inalaani ghasia na machafuko
2014 Oct 19 , 11:33
Jaji wa Mahakama Kuu ya mji wa Lagos nchini Nigeria ametetea na kuungamkono marufuku iliyokuwa imetangazwa kwa vazi la hijabu ya Kiislamu kwa shule za serikali katika mji huo.
2014 Oct 19 , 07:04
Jumuiya ya Wanazuoni na Wakufunzi wa Chuo Kikuu cha Kidini cha mji mtakatifu wa Qum nchini Iran imelaani hukumu ya kifo iliyotolewa na mahakama moja ya Saudi Arabia dhidi ya mwanazuoni mkubwa wa nchi hiyo Ayatullah Nimr Baqir al Nimr na imetoa wito wa kuachiwa huru msomi huyo bila ya masharti yoyote.
2014 Oct 17 , 09:51
Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, harakati hiyo imeazimia kupambana na makundi ya kitakfiri na magaidi licha ya mashinikizo yanayoikabili nchi hiyo hivi sasa.
2014 Oct 14 , 20:19
Kundi la Waislamu wa mji wa Buffalo katika jimbo la New York huko Marekani imewagawia wananchi wa mji huo mashada ya maua yenye semi na maneno ya Mitume wa dini za mbinguni.
2014 Oct 14 , 20:04