Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema hayo leo katika hadhara ya maafisa wa ngazi za juu wa Mfumo wa Kiislamu, mabalozi wa nchi za Kiislamu hapa Tehran na kundi la familia za Mashahidi kwa mnasaba wa maadhimisho ya Mab'ath na kupewa Utume Mtume Muhammad SAW na kubainisha kwamba, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ikiwa mstari wa mbele katika harakati ya kusukuma mbele gurudumu la Mab'ath iliayoanzishwa na Imam Ruhullah Khomeini MA, itaaendelea na njia yake hiyo bila ya kuogopa madola yenye nguvu duniani.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa mkono wa kheri, baraka na fanaka kwa Umma wa Kiislamu na taifa kubwa la Iran na kueleza kuwa, Siku kuu ya Maba'th ni Idi ya mwamko na harakati na siku ya kurejea katika fitra ya Mwenyezi Mungu na maisha yanayoambatana na utumiaji akili, uhuru, uadilifu na uja kwa Mwenyezi Mungu.
Ayatullah Khaemenei amesema kuwa, jukumu la Mitume wa Mwenyezi Mungu lilikuwa ni kuwaongoza wanadamu kuelekea katika fitra na maumbile haya masafi katika kalibu ya maamrisho ya Mwenyezi Mungu na Tawhidi (kumpwekesha Mwenyezi Mungu).
Ayatullah Khamenei amesema kuwa, harakati ya Uzayuni inayotawala dunia ni mfano wa wazi wa uundaji mfumo wa mashetani na kwamba, hali ya leo ya dunia ni matokeo ya mtandao mpana wa mabepari wa Kizayuni.
Aidha Ayatullah Khamenei amesema, Marekani inachochea chuki dhidi ya Uislamu, chuki dhidi ya Iran na chuki dhidi ya madhehebu ya Shia.Katika mkutano huo, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
ameashiria kuendelea kuwepo mapambano baina ya mrengo wa mab'ath na
Utume na mrengo wa ujahilia tangu mwanzoni mwa kudhihiri dini tukufu ya
Kiislamu hadi leo hii na kusema kuwa, vielelezo vikuu vya mrengo wa
mab'ath na Utume ni hekima na busara kubwa iliyoongozwa na Bwana Mtume
wa Mwenyezi Mungu SAW na kielelezo kikuu cha mrengo wa ujahilia ni
uasherati na ghadhabu na kuongeza kuwa: Jukumu kuu la umma wa Kiislamu
leo hii ni kukabiliana na mrengo wa ujahilia unaoongozwa na Marekani na
kwa upande wake, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambayo iko mstari wa mbele
katika mrengo wa kushikamana na mafundisho ya Mtume Muhammad SAW,
itaendelea na njia yake iliyoanzishwa na Imam Khomeini (quddisa sirruh)
ya kupambana na kukabiliana vilivyo na madola ya kibeberu bila ya woga
wowote.
Ayatullah Udhma Khamenei aidha ametoa mkono wa baraka kwa
mnasaba kuadhimisha siku ya kubaathiwa na kupewa Utume Mtume Muhammad
SAW kwa umma wa Kiislamu na kwa taifa kubwa la Iran na huku akitoa
ushahidi kutoka katika aya za Qur'ani Tukufu amezungumzia maana pana na
ya kina sana na kubaathiwa Bwana Mtume akisema: Siku ya kubaathiwa ni
sikukuu adhimu na ni siku ya kurejea kwenye maumbile aliyoumbwa nayo
mwanadamu na kuishi katika maisha ya hekima, mantiki, ukombozi, uadilifu
na unyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu na kwamba kazi ya Mitume wa Mwenyezi
Mungu ni kuwaongoza wanadamu kuelekea kwenye maumbile hayo safi na
kutakafari maumbile ya Mwenyezi Mungu na kutenda kila jambo kwa
kuzingatia maamrisho ya Allah Mtukufu na kushikamana na tawhidi.
Vile
vile ameashiria namna mwanadamu anavyohitajia muda wote mafundisho ya
Mtume na kuutaja mrengo wa ujahilia kuwa ni kambi inayokinzana
kikamilifu na mafundisho hayo ya Mtume. Ameongeza kuwa: Mrengo wa
ujahilia hauhusiani tu na zama za Bwana Mtume Muhammad SAW, bali ni
mrengo uliondelea kuwepo hadi leo hii ukikabiliana na mrengo wa
kutafakari maumbile ya Mwenyezi Mungu unaoongozwa na mafundisho ya Bwana
Mtume Muhammad SAW ingawa leo hii mrengo huo wa ujahilia unatumia elimu
na teknolojia ya zama hizi kuendeleza vita vyake kwa sura nyingine
tofauti na ile ya zama za Bwana Mtume.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi
ya Kiislamu amesisitiza kuwa, uasherati, ghadhabu na hawaa za nafsi
ndivyo vielelezo vikuu vya mrengo wa ujahilia na kuongeza kuwa: Matokeo
ya vitendo vya kambi ya ujahilia siku zote ni mateso, matatizo,
kumdhalilisha mwanadamu, kuua mamilioni ya watu, kupora mali za mataifa
mengine na kueneza ufisadi duniani ambapo mfano wa wazi kabisa wa suala
hilo ni vita viwili vikubwa vya kimataifa.
Ayatullah Udhma Khamenei
amegusia pia suala la kuzuka mirengo miwilli ya ujahilia na ule wa
mafundisho ya Mtume Muhammad SAW katika upeo wa watu binafsi, wa kijamii
na kimataifa na kuongeza kuwa: Kama katika upeo wa kimataifa mienendo
ya madola yenye nguvu itaongozwa kwa busara za mafundisho ya Bwana Mtume
SAW bila ya shaka yoyote dunia itakuwa kwa sura nyingine tofauti na
itakavyokuwa wakati miamala na vitendo vya madola yenye nguvu
vitakapoongozwa na hawaa za nafsi, kupenda ukubwa na kueneza fitna
duniani.
Amesema, kukandamizwa mataifa ya dunia na madola ya kikoloni
ni mfano mwingine wa wazi wa vitendo vya mrengo wa kijahilia na huku
akiashiria madhara makubwa iliyopata India kutokana na ukoloni wa makumi
ya miaka wa dola la kikoloni la Uingereza, amesema kuwa: Vita na fitna
zilizoenea leo katika eneo la magharibi mwa Asia ni matokeo mengine ya
vitendo vya kambi ya kijahilia na ya shetani.
Kiongozi Muadhamu wa
Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza pia kuwa, mrengo wa Uzayuni unaotawala
dunia hivi sasa ni mfano mwingine wa wazi wa mfumo wa mashetani na
kusema: Hali ilivyo duniani leo ni matokeo ya kutawaliwa dunia na kanali
pana ya mabepari wa Kizayuni ambao wamepenya na wana nguvu hadi ndani
ya serikali kama ya Marekani na kwamba mrengo na chama chochote kile
hakiwezi kupata nguvu na kuingia madarakani katika nchi hizo bila ya
kuwa mfuasi wa mrengo huo wa Kizayuni.
Ayatulllah Udhma Khamenei
ameutaja msingi mkuu wa harakati adhimu ya Umma wa Kiislamu na Iran
pamoja na mwamko wa Kiislamu, kuwa ni kupambana na nguvu za mrengo huo
fasidi wa Kizayuni na kuongeza kusema kwamba: Ni kwa sababu hiyo ndio
maana leo hii siasa za kueneza chuki dhidi ya Uislamu, dhidi ya Iran na
dhidi ya Ushia zikawa ndizo sera kuu na zisizobadilika za Marekani na
tawala zenye mfungano na dola hilo la kibeberu.
Vile vile ameutaja
mwamko na kuwa macho taifa la Iran na mataifa ya Kiislamu katika
kukabiliana na harakati za kiharibifu na kifisadi za madola ya kibeberu
kuwa ndiyo sababu kuu inayoyahamakisha madola hayo ya kiistikbari na
kuongeza kuwa: Ni kwa sababu hiyo ndio maana Iran kutokana na kupinga
siasa za Marekani katika eneo hili, inafanyiwa vitisho vya kila namna na
inawekewa vikwazo na mashinikizo kwani madola hayo yanajua kuwa Jamhuri
ya Kiislamu inahatarisha manufaa ya siasa zao za kibeberu za kupenda
kujikumbizia kila kitu upande wao.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya
Kiislamu amesisitiza kuwa, matokeo ya kutawala kambi ya kijahilia na
madola ya kishetani ni kuenea maovu na utaghuti duniani na kuongeza
kuwa: Pamoja na kwamba mrengo wa ujahilia na wa kitaghuti ulitumia bomu
la atomiki kuua mamia ya maelfu ya watu huko Hiroshima (Japan) lakini
baada ya kupita miaka mingi hadi leo hii unaendelea kufanya ukaidi na
hautaki kuomba radhi kwa jinai yake hiyo kama ambavyo pia unaangamiza
miundombinu ya nchi za Iraq na Afghanistan bila ya kujali chochote wala
kujirudi moyoni.
Ayatullah Udhma Khamenei amesisitiza kuwa: Jamhuri
ya Kiislamu ya Iran kamwe si mwanzishaji wa vita wala si mfanyaji wa
harakati za kijeshi dhidi ya nchi yoyote ile lakini inasimamia na
kulinda misimamo yake kwa sauti kubwa na itaendelea kufanya hivyo.
Ameashiria
pia istilahi ilizokuwa zikitumiwa na Imam Khomeini (quddisa sirruh)
kama vile fikra mgando kwa jina la Uislamu sambamba istilahi ya Uislamu
wa Kimarekani na kuziweka istilahi hizo mbili katika mkabala wa istilahi
ya Uislamu wa kweli na kuongeza kuwa: Makundi fasidi na yanayofanya
ufisadi na uharibifu katika ardhi ambayo leo hii yanafanya jinai mbaya
kabisa na ukatili wa kuchupa mipaka kwa jina la Uislamu, yanaungwa mkono
na kusaidiwa kikamilifu na madola ya Magharibi.
Kiongozi Muadhamu wa
Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa: Wamagharibi wamejifanya kuunda
muungano wa kupambana na Daesh (ISIS) lakini kwa hakika ni waungaji
mkono wa genge hilo na wanafanya hivyo kwa makusudi ili kuendelea
kuupiga vita Uislamu huku katika propaganda zao wakishikilia kutumia
neno dola la Kiislamu kila wanapozungumzia kundi hilo kwa lengo la
kuipaka matope sura ya Uislamu.
Ayatullah Udhma Khamenei amegusia pia
suala la kuenea na kuzidi kupata nguvu harakati ya Kiislamu licha ya
kuweko vita hivyo vikubwa vya mrengo wa ujahilia dhidi ya Uislamu na
kusema kuwa: Harakati ya Kiislamu ambayo ilipata nguvu na kuimarika
baada ya kuundwa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu nchini Iran itaendelea na
harakati zake na bila ya shaka yoyote itashinda tu.
Vile vile
amesisitizia ulazima wa kutawakali kwa Mwenyezi Mungu na kutoogopeshwa
na njama na vitisho vya madola ya kibeberu na kuongeza kuwa: Leo hii
umma wote wa Kiislamu, iwe ni watu wa kawaida, au watu wenye vipawa au
viongozi; kila mmoja ana jukumu - mbele ya harakati ya Kiislamu - la
kukabiliana na mrengo huo wa ujahilia na kama kila mmoja atatekeleza
majukumu hayo vizuri na kwa njia ipasayo basi atapata malipo na thawabu
kutoka kwa Mwenyezi Mungu na mtu yeyote ambaye hatatekeleza vizuri
majukumu yake, (hasara itakuwa kwake yeye mwenyewe lakini) harakati ya
Kiislamu haitakwama bali itaendelea na njia yake, kwani hatima ya yote,
ni Uislamu na Waislamu ndio watakaoshinda tu.
Kabla ya hotuba ya
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Hujjatul Islam Walmusilimia
Hassan Rouhani, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa mab'ath
ni siku ya rehema kwa viumbe wote na kuongeza kuwa: Rehema za Mtume wa
Uislamu SAW si kwa ajili ya Waislamu tu, bali mtukufu huyo ni dhihirisho
la rehema kwa wanadamu wote kwani ametumwa kuja kuwaonesha wanadamu
wote njia ya uongofu.
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amegusia
tuhuma zinazotolewa leo hii duniani dhidi ya Uislamu kwa kuihusisha dini
hiyo ya Mwenyezi Mungu na vitendo vya kigaidi na ukatili na kusema
kuwa: Wale watu ambao leo hii wameanzisha wimbi kubwa la vita dhidi ya
Uislamu bila ya insafu, wanapaswa siku moja angalau wafanye uadilifu wa
kuuangalia Uislamu kwa jicho zuri ili waweze kupata funzo kutokana na
uadilifu uliofanywa na Mtume Muhammad SAW kwa washirika na watu
waliokuwa wanakana kuwepo Mwenyezi Mungu.
Rais Hassan Rouhani
ameongeza kuwa: Kwa upande mmoja, leo hii kuna vita na chuki za
Wamagharibi ambao kwa karne nyingine wamekuwa wakiendesha propaganda
dhidi ya Uislamu na kwa upande mwingine kuna marafiki wajinga au mamluki
wanaotumiwa vibaya na Wamagharibi na kwa hakika hizo ni pande mbili za
makali za mkasi unaolichana jina zuri la Uislamu.
Rais Hassan Rouhani
aidha ameuliza swali akisema, ni nani aliyeleta ugaidi na ukosefu wa
amani katika eneo la Mashariki ya Kati na kuanzisha utawala ghasibu na
dhalimu (wa Kizayuni) miaka 70 iliyopita? Amesema: Chanzo cha ukosefu
mkubwa wa amani, ugaidi na vita vya mara kwa mara vinavyojiri katika
eneo la Mashariki ya Kati, ni utawala wa Kizayuni (wa Israel) unaoikalia
kwa mabavu Quds tukufu.
Vile vile ameashiria suala la kukaliwa kwa
mabavu Afghanistan na kuvamiwa Iraq pamoja na kuzushwa ukosefu wa amani
katika eneo la Mashariki ya Kati na kusema kuwa: Wahusika wa jinai zote
hizo ni Wazayuni na Wamarekani.
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
aidha amesema, lengo kuu na la mwisho la mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ni
kuleta amani na usalama katika kona zote za dunia na kuhoji kwa kusema:
Tutaweza vipi kukaa kimya wakati wananchi wa Yemen kila leo
wanashambuliwa kinyama kabisa na watu ambao wanajinadi kuwa ni wafawidhi
na wahudumu wa Masjidul Haram?
Rais Rouhani amesisitiza kuwa:
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaona fakhari - chini ya miongozo ya busara
ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu - kuwatetea na kuwahami
watu wanaochulumiwa na itaendelea kufanya hivyo katika siku za usoni.
Amesema: Popote itakapolazimu, tutatekeleza amri za Amirijeshi wetu Mkuu
katika kuwasaidia na kuwa pamoja na watu wanaodhulumiwa popote pale
ulimwenguni.