IQNA

Khitma ya Marhum Sheikh Abdillahi Nassir yafanyika Qum, Iran

9:48 - January 17, 2022
Habari ID: 3474817
TEHRAN (IQNA)- Khitma ya Marehemu Hajj Sheikh Abdullahi Nassir Juma Bhalo, mwanazuoni mashuhuri wa Kiislamu na kiongozi wa kimaanawi wa Waislamu wa madhehebu ya Shia Afrika Mashariki imefanyika katika Msikiti wa Imam Ja'far Sadiq AS katika Chuo Kikuu cha Al-Bayt AS katika mji mtakatifu wa Qum.

Khitma hiyo iliyofanyika Jumapili Januari 16 imeandaliwa na wanafunzi wa Kenya mjini Qum, kwa ushirikiano na baadhi ya taasisi za kimataifa - ikiwa ni pamoja na Jumuiya ya Kimataifa ya  Ahl al-Bayt AS, Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al-Mustafa SAW na Mahdi TV.

Wanafunzi Waafrika na wanazuoni wa ngazi za juu wa nchini Iran wameshiriki katika majlisi hiyo huku hali ya huzuni ikionekana imetanda miongoni mwa washiriki kutokana na kumpoteza mwanazuoni huyo mkubwa ambaye itakuwa vigumu kujaza pengo lake.

Akizungumza katika kikao hicho, Hujjatul Islam wal Muslimin Mohammad Salim, mmoja kati ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa SAW ameanza kwa kutuma salamu za rambi rambi katika mnasaba wa kukumbuka kuaga dunia Ummul Banin SA na pia kufuatia kuaga dunia Sheikh Abdillahi Nassir na kusema: "Yamkini wengi  duniani hawakuweza kumjua Sheikh Abdillahi Nassir ambaye alikuwa mwanamapambano katika njia ya Mwenyezi mungu lakini katika ukanda wa Afrika Mashariki na hasa nchini Kenya, Waislamu walikuwa wanamfahamu vyema."

Naye Hujjatul Islam wal Muslimin Sheikh Salim Mwega, mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa SAW amemtaja Sheikh Abdillahi Nassir kuwa mwanamapambano ambaye hakuchoka na jina lake ni mashuhuri kote Kenya na Afrika Mashariki kwa ujumla. Sheikh Mwega amesema katika umri wake wote, marhum Sheikh Abdillahi Nassir daima alikuwa mtetezi wa uadilifu na kuongeza kuwa: "Sheikh Abdillahi Nassir alikuwa miongoni mwa wapigania ukombozi wa Kenya na alifanikiwa katika jitihada zake hizo kwa kushirikiana na wananchi."

Aidha amesema marhum Sheikh Abdillahi Nassir pia alikuwa na nafasi muhimu katika maombolezo ya siku 11 ambayo hufanyika mwezi wa Muharram maeneo mbali mbal nchini Kenya. Amebaini kuwapamoja na kuwepo njama za maadui, marhum aliweza kufanikisha harakati adhimu ya wananchi katika maombolezo ya siku ya Ashura nchini Kenya.

Sheikh Abdillahi Nassir Juma Bhalo, msomi maarufu wa Kiislamu barani Afrika na hasa Afrika Mashariki aliaga dunia mapema Januari 11 mjini Mombasa, Kenya.

Mwanazuoni huyu mtajika aliandika vitabu mbalimbali kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza, vilivyosaidia pakubwa kujenga na kukuza imani za Waislamu. Baadhi ya vitabu hivyo vimefasiriwa kwa kadhaa za kigeni.

Katika miaka ya karibuni amekuwa akijishughulisha na uandishi wa tafsiri ya Qur’ani Tukufu kwa lugha ya Kiswahili na kueneza mafundisho ya Ahlul Bayyt (as). Miongoni mwa vitabu vya marehemu Sheikh Abdillahi Nassir ni Shia na Qur'ani, Maulidi si Bidaa, Si Haramu, Ukweli wa Hadithi ya Kisaa, Mut'a Ndoa Halali, Ukweli wa Hadithi ya Karatasi, Ahlul Bayt Ni Nani? na Yazid Hakuwa Amirul Muuminin.

Vikao mbali mbali vya Khitma ya marhum Sheikh Abdillahi Nassir vinaendelea kufanyika Kenya na Tanzania na maeneo mengine duniani.

آیین بزرگداشت رهبر معنوی شیعیان شرق آفریقا برگزار شد

آیین بزرگداشت رهبر معنوی شیعیان شرق آفریقا برگزار شد

4029109

captcha