IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Morocco kufanyika kufanyika mwezi huu

18:10 - September 04, 2022
Habari ID: 3475730
TEHRAN (IQNA) - Mashindano ya 16 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Morocco yataandaliwa baadaye mwezi huu.

Mji wa magharibi wa Casablanca utakuwa mwenyeji wa hafla ya Qur'ani Tukufu mnamo Septemba 27-28, Wizara ya Masuala ya Kiislamu ya Morocco na Wakfu ilisema.

Washindani watashindana katika kuhifadhi Qur'ani, usomaji wa Tarteel, Tajweed na Tafseer (Tafsiri ya Qur'ani), iliongeza.

Mashindano hayo yatafunguliwa asubuhi Jumanne, Septemba 27, katika shule ya Qur'ani inayohusishwa na Msikiti wa Hassan II.

Kwa mujibu wa wizara hiyo, wahifadhi na wasomaji Qur'ani kutoka nchi za Kiarabu na Kiislamu za Asia na Afrika pamoja na nchi kadhaa za Ulaya zitashiriki katika mashindano hayo.

Ilisema mashindano hayo yanafanyika kwa mnasaba wa kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtukufu Mtume (SAW) kama sehemu ya juhudi za wizara ya kuendeleza kuhifadhi Qur'ani, Tajweed na Tafseer.

Morocco ni nchi ya Kiarabu ya Kaskazini mwa Afrika inayopakana na Bahari ya Atlantiki na Bahari ya Mediterania. Uislamu ndiyo dini kuu nchini Morocco, huku asilimia 99 hivi ya watu wakiufuata.

3480320

captcha