IQNA

Waislamu Australia

Waislamu Australia wapongeza marufuku ya Unyanyasaji wa Kidini

20:48 - August 27, 2023
Habari ID: 3477503
CANBERRA (IQNA) – Sajili ya Vitendo vya Chuki Dhidi ya Uislamu Australia (IRA) imepongeza marufuku ya udhalilishaji kidini huko New South Wales.

IRA ilianzishwa mnamo Septemba 2014 kwa kujibu vitendo vinavyoongezeka vya  chuki dhidi ya Uislamu.

Sajili ya Vitendo vya Chuki Dhidi ya Uislamu Australia (IRA) imesema inakaribisha sheria muhimu katika NSW inayokataza kuvunjiwa heshima kidini, katika mfumo wa marekebisho ya Sheria ya Kupambana na Ubaguzi ya NSW ya 1977, ambayo hatimaye imepitishwa na bunge la New South Wales.

Sheria inafanya kuwa ni kinyume cha sheria, " kuchochea chuki dhidi ya, dharau kubwa, au dhihaka kali kwa mtu au kikundi cha watu, kwa sababu ya imani yao ya kidini, ushirika au shughuli".

IRA imeendelea kusema: "Tunaamini kwamba jumuiya ya Kiislamu iko katika hatari kubwa ya kudhalilishwa kidini kwa sababu Waislamu ni kundi la pili kwa ukubwa la imani nchini Australia kufuatia Ukristo."

Wanawake wengi wa Kiislamu huvaa Hijabu, na kwa bahati mbaya, chuki dhidi Uislamu unawaathiri sana wanawake kwa sababu ni rahisi kutambua Imani yao kutokana na vazi lao ls staha la Hijabu..

Ripoti ya hivi punde zaidi ya Sajili ya Vitendo vya Chuki Dhidi ya Uislamu Australia (IRA) iliyochapishwa Machi 2023 kwa ushirikiano na Chuo Kikuu cha Charles Sturt (CSU) na Chuo cha Utafiti wa Sayansi ya Kiislamu (ISRA) na iliyoandikwa na Dk Derya Iner, ilifichua kuwa kati ya majimbo na wilaya zote za Australia, idadi kubwa zaidi ya vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu vilijiri New South Wales.

Ripoti hiyo pia ilifichua kuwa asilimia 78 ya wahanga wa matukio ya chuki dhidi ya Uislamu walikuwa wanawake.

Kwa msingi huo sheria hii ni hatua muhimu kwani itapunguza matukio ya chuki dhidi ya Uislamu. Hatahivyo IRA inasisitiza ulazima wa kuwa macho na kuendelea kuripoti matukio ya chuki dhidi ya Uislamu nchini Australia.

Habari zinazohusiana
captcha