IQNA

Ulimwengu wa Kiislamu

Klipu ya Watoto wa Morocco wakisoma Qur’ani yasambaa mitandaoni

20:43 - September 14, 2023
Habari ID: 3477595
RABAT (IQNA) – Klipu ya video inayoonyesha usomaji wa Qur’ani Tukufu watoto nchini Morocco katikaeneo lililokumbwa na tetemeko la ardhi lililosababishauharibifu mkubwa hivi majuzi imesambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Watoto wanaonekana wakisoma aya za Qur’ani Tukufu baada ya kupokea msaada wa serikali uliotumwa katika maeneo yaliyokumbwa na tetemeko hilo.

Watumiaji wa mitandao ya kijamii wamewapongeza watoto hao na kueleza hatua yao hiyo kuwa ni kielelezo cha elimu yao ya kidini na tabia njema za kimaadili.

Pia wametaka msaada zaidi kutumwa katika maeneo yaliyoathiriwa na tetemeko hilo.

Idadi ya waliofariki kutokana na tetemeko baya zaidi la ardhi nchini Morocco katika zaidi ya miongo sita imeongezeka na kufikia zaidi ya 2,900, huku waokoaji wakipambana na wakati kutafuta manusura.

Tetemeko hilo la ukubwa wa 6.8 katika kipimo cha Richter lilitokea Ijumaa Agosti nane katika Milima ya ya Atlas, na kitovu hicho kikiwa kilomita 72 (maili 45) kusini magharibi mwa Marrakech.

Waokoaji walisema nyumba za jadi za matofali ya udongo zilizoenea katika eneo hilo zilipunguza uwezekano wa kupata manusura kwa sababu zilikuwa zimebomoka.

captcha