Sala hiyo iliongozwa na Ayatullah Seyyed Ali Khamenei, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu. Sala hiyo ilihudhuriwa na maafisa wakuu wa mihimili ya dola nchini Iran pamoja na makamanda wa kijeshi,wananchi wa matabaka mbali mbali na wanadiplomasia wa kigeni.
Sala ilisaliwa saa mbili unusu asubuhi, lakini umati wa watu ulianza kufika katika uwanja huo mkubwa wa Swala mapema Alfajiri.
Mapema Siku ya Jumanne, Iran ilitangaza kwamba baada ya kuonekana kwa mwezi, Jumatano itakuwa sikukuu ya Idul Fitr. Hii ni siku ambayo huadhimisha mwisho wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, ambao huwa na siku 29 au 30.
Katika nchi nyingi za Kiislamu na hata zisizo na Kiislamu, ikiwa ni pamoja na Iran, kamati za kutazama mwezi huundwa ili kuthibitisha kuanza kwa mwezi wa Shawwal.
4209700