Ghasia na machafuko mapya yamezuka kati ya askari wa utawala wa kizayuni wa Israel na waandamanaji wa Palestina katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu na Israel baada ya utawala huo kufunga Msikiti mtukufu wa al Aqsa.
2014 Nov 06 , 10:21
Katibu Mkuu wa Harakatiya Hizbullah nchini Lebanon amesema kuwa, machafuko na migogoro inayoendelea kushuhudiwa katika eneo la Mashariki ya Kati haifungamani kabisa na Ushia wala Usuni, bali ni mkakati maalumu wa Marekani wenye lengo la kutaka kulidhibiti eneo hili nyeti.
2014 Nov 04 , 19:20
Sheikh Bilal Shaaban Katibu Mkuu wa chama cha Hizb Tauhid Islami nchini Lebanon amejiunga na wapenda uhuru na haki duniani katika kulaani vikali hatua ya utawala wa Kizayuni wa Israel kufunga milango ya Msikiti wa Al Aqsa na kuwazuia Waislamu kuswali ndani ya msikiti huo.
2014 Nov 01 , 16:34
Utawala haramu wa Kizayuni, kwa mara ya kwanza leo Ijumaa alfajiri umefungua milango ya Msikiti wa al-Aqsa baada ya kuifunga mwaka 1967. Utawala huo pia umeshadidisha ulinzi katika maeneo ya jirani na msikiti huo, kutokana na hofu ya kuzuka mapambano makali kutoka kwa Wapalestina.
2014 Oct 31 , 16:14
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei, amesema kuwa, ibada ya hija ni fursa bora kabisa kwa ajili ya kukabiliana na njama za kuitenganisha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na ulimwengu wa Kiislamu na nara yake ya ‘kukabiliana na shubha na propaganda zinazoenezwa na maadui wa Uislamu’ na kutoa jibu mwafaka kwa mahitaji ya kimaanawi na kifikra za mahujaji.
2014 Oct 28 , 21:40
Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah nchini Lebanon amesema kuwa watu wanaofikiri kwamba kwa kuanzisha vita vya kisaikolojia na vitisho wataweza kuzuia kufanyika maombolezo ya Aba Abdillah Imam Hussein AS wanajidanganya, kwani vitisho hivyo havitawatenganisha na Imam Hussein AS.
2014 Oct 26 , 09:39
Katika sala ya Ijumaa Tehran
Khatibu wa Swala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa mjini Tehran ameionya Saudia Arabia kuhusiana na hukumu ya kifo dhidi ya mwanazuoni mashuhuri wa Kishia nchini humo Ayatullah Sheikh Nimr Baqir al-Nimr.
2014 Oct 25 , 11:23
Tajiri maarufu wa Saudi Arabia Al Waleed bin Talal amekiri kuwa nchi hiyo ya kifalme inawasaidia magaidi wa kundi la kigaidi la Daesh (ISIL) ambalo linapigana dhidi ya serikali za Iraq na Syria.
2014 Oct 25 , 11:09
Viongozi wa ngazi za juu na wananchi wa matabaka mbalimbali Alkhamisi walishiriki kwenye mazishi ya Ayatullah Mohammad Ridha Mahdavi Kani, aliyekuwa Mkuu wa Baraza la Wanazuoni Wataalamu Wanaomchagua Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika Haram ya Hadhrat Abdul Adhim Hassani AS, katika kitongoji cha Shahr Rey, nje kidogo ya jiji la Tehran
2014 Oct 23 , 13:16
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haina imani kwamba, wale wanaodai kuendesha mapambano dhidi ya kundi la kigaidi la Daesh (ISIL) katika eneo wana nia ya dhati juu ya suala hilo.
2014 Oct 22 , 21:52
Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon, Sayyid Hassan Nasrullah amesema, migogoro inayoendelea hivi sasa Mashariki ya Kati ina lengo la kuchora upya ramani ya eneo hili.
2014 Oct 21 , 20:05
Mahmoud Abbas Mkuu wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina ameahidi kuchukua hatua za kisheria kuzuia walowezi wa Kizayuni kuuvuamia Msikiti wa Al Aqsa katika Baitul Muqaddas.
2014 Oct 20 , 11:06
Misikiti na vituo vya Kiislamu katika mji wa la Inland ndani ya jimbo la California, vimeendelea na juhudi zao za kuwafahamisha watu kuhusu Uislamu wa asili ambao unapenda amani na utulivu.
2014 Oct 17 , 23:18