Misikiti na vituo vya Kiislamu katika mji wa la Inland ndani ya jimbo la California, vimeendelea na juhudi zao za kuwafahamisha watu kuhusu Uislamu wa asili ambao unapenda amani na utulivu.
2014 Oct 17 , 23:18
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa ushindi wa Ghaza wa mapambano katika vita vya siku 50 na matamshi ya kushindwa utawala wa Kizayuni mbele ya raia waliozingirwa ni ushindi mkubwa na dhihirisho la ahadi na msaada wa Mwenyezi Mungu na ni bishara ya kufikia ushindi mkubwa zaidi.
2014 Oct 17 , 21:01
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetangaza kuchukizwa mno na matamshi yaliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Saudi Arabia dhidi ya Iran.
2014 Oct 14 , 14:26
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullahil-Udhmaa Sayyid Ali Khamenei amesema kuwa, hatua yoyote inayochochea chuki na tofauti baina ya Suni na Shia, inaisaidia Marekani, Uingereza na utawala haramu wa Kizayuni, yaani katika kuibua harakati za kijinga, zilizopitwa na wakati na za kitakfiri.
2014 Oct 14 , 14:20
Khatibu wa Sala ya Idul Adh'ha iliyosaliwa Jumapili asubuhi kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha Tehran amesema kuwa, iwapo Waislamu wataitumia vizuri ibada ya Hija, wakaamka na kuzitambua vizuri njia za kukabiliana na adui, kamwe Umma wa Kiislamu hautadhalilishwa.
2014 Oct 06 , 23:04
Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo mjini Tehran amesema kuwa, wananchi wa Iran wanaunga mkono mazungumzo ya nyuklia kati ya serikali na kundi la 5+1 sanjari na kuchungwa mistari myekundu ya Jamhuri ya Kiislamu.
2014 Oct 03 , 20:19
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei ametoa ujumbe wa kila mwaka wa Hija kwa Mahujaji wa Nyumba ya Mwenyezi Mungu, ambapo amesema Miongoni mwa masuala muhimu na yanayostahiki kupewa kipaumbele kikubwa zaidi hivi sasa ni suala la mshikamano na umoja wa Waislamu.
2014 Oct 03 , 13:01
Sayyid Hassan Nasrullah Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema kipaumbele cha kwanza cha Hizbullah ni kukabiliana vikali na makundi ya kigaidi na kitakfiri na kuzuia kuenea machafuko nchini Lebanon.
2014 Oct 01 , 22:26
Waziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) ameyashambulia vikali makundi ya kigaidi na kitakfiri katika eneo la Mashariki ya Kati akisema kuwa makundi hayo yanaonyesha picha mbaya kwa dini tukufu ya Kiislamu.
2014 Sep 30 , 00:03
Katibu Mkuu wa chama cha Hizbullah cha Lebanon amesema kuwa Marekani haina ustahiki wa kiakhlaqi wa kuendesha mapambano dhidi ya ugaidi. Sayyid Hassan Nasrullah ameyasema hayo kupitia hotuba aliyoitoa jana usiku.
2014 Sep 27 , 12:54
Katibu Mkuu wa Muungano wa Maulamaa wa Kiislamu Duniani amelitaka kundi la kigaidi la Daesh kuacha mara moja kutenda jinai dhidi ya wanadamu.
2014 Sep 27 , 12:52
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei asubuhi ya leo ameruhusiwa kuondoka katika Hospitali ya Shahid Rajai mjini Tehran baada ya kukamilisha matibabu na kupata nafuu kikamilifu.
2014 Sep 15 , 20:07
Mufti wa Quds na Ardhi za Palestina Sheikh Muhammad Hussein amesema kuwa kundi la kigaidi la Daesh limefanya matendo yanayopotosha sura ya Uislamu na ni tishio kwa Umma wa Kiarabu na Waislamu.
2014 Sep 15 , 20:03