Mwanazuoni mmoja wa Chuo Kikuu cha Al Azhar nchini Misri amesema kuwa makundi ya Mawahabi na Matakfiri wanaoipinga serikali ya Syria wanapata himaya ya nchi za Magharibi.
2014 May 10 , 17:27
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei amesema shughuli za ustawi na utafiti wa nyuklia Iran kamwe hazitasimamishwa.
2014 Apr 10 , 14:16
Kundi lenye misimamo mikali ya Kikristo la Anti Balaka sasa limeanza kutumia mbinu mpya kwa ajili ya kuua Waislamu katika Jamhuri ya Afrika ya Kati kwa kuwauzia vyakula vyenye sumu. Hadi sasa makumi ya watoto wadogo wameripotiwa kufariki dunia katika mji wa Buda kutokana na mbinu hiyo ya mauaji.
2014 Apr 09 , 17:28
Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC imesema itaunga mkono ombi la Palestina kwa Umoja wa Mataifa kujiunga na na mikataba 15 ya kimataifa.
2014 Apr 06 , 10:13
Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu,Hizbullah, nchini Lebanon amesema iwapo wanamapambano wa harakati hiyo wasingeliingia nchini Syria, makundi ya kigaidi na kitakfiri yangeliwanyanyasa wananchi wote wa Lebanon.
2014 Mar 30 , 18:16
Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu yaani Bunge laa Iran amesema kuwa uzoefu wa miaka mingi iliyopita umeonesha kwamba ugaidi na ubeberu ni ncha mbili za mkasi unaotishia Umma wa Kiislamu na kwamba watu wa Iraq, Syria, Afghanistan na Pakistan wamehisi zaidi machungu ya mkasi huo kuliki watu wa maeneo mengine.
2014 Feb 19 , 12:53
Rais Hassan Rouhani wa Iran ametoa wito kwa nchi za Kiislamu kudumisha umoja ili kuweza kukabiliana na vitisho visivyo na kifani.
2014 Feb 18 , 19:26
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei Jumatatu alihutubia maelfu ya wananchi wa miji mbalimbali ya mkoa wa Azarbayjan Mashariki waliokwenda kuonana naye akilishukuru taifa la Iran kwa kujitokeza kwa wingi katika maandamano ya tarehe 22 Bahman (Februari 11) ya kuadhimisha miaka 35 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu hapa nchini.
2014 Feb 18 , 13:22
Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa harakati ya muqawama wa Kiislamu ya Lebanon Hizbullah, amekosoa kughafilika kwa nchi za Kiislamu juu ya hatari ya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel ambao ni tishio kwa Lebanon, palestina na ulimwengu mzima.
2014 Feb 17 , 16:54
Wizara ya Awqaf na Masuala ya Kidini nchini Misri imeandaa semina yenye anuani ya ‘Hatari ya Fikra za Kitakfri’.
2014 Feb 16 , 08:58
Shirika Kubwa la Bima (re-insurance au bima mara ya pili) ya Kiislamu linatazamiwa kuanzishwa Kenya baadaye mwaka huu kwa lengo la kutoa huduma kwa mashirika ya bima ya Kiislamu ijulikanayo kama Takaful nchini humo.
2014 Feb 13 , 13:30
Shirika la Msamaha Duniani la Amnesty International limeonya kuwa kuna operesheni za kufukuza jamii ya Waislamu kwa kuwaua kwa umati katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, suala ambalo askari wa kulinda amani wa kimataifa wameshindwa kulizuia.
2014 Feb 13 , 13:24
Mkuu wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu amesema kuhusiana na mazungumzo ya nyuklia kati ya Iran na mataifa sita yenye nguvu duniani kwamba, mazungumzo hayo yanaweza kutatua masuala yote kama nchi za Magharibi zitaacha kutoa visingizio.
2014 Feb 10 , 11:23