Mkuu wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu amesema kuhusiana na mazungumzo ya nyuklia kati ya Iran na mataifa sita yenye nguvu duniani kwamba, mazungumzo hayo yanaweza kutatua masuala yote kama nchi za Magharibi zitaacha kutoa visingizio.
2014 Feb 10 , 11:23
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuzuia unyanyasaji na mauaji ya Waislamu duniani ndio jukumu kuu la Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC).
2014 Feb 07 , 10:57
Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu imetangaza kuwa Kongamano la Kimataifa la Umoja wa Kiislamu litafanyika mjini Tehran Januari 17.
2013 Dec 07 , 12:55
Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC imelaani na kukosoa vikali uamuzi wa serikali ya Angola wa kuipiga marufuku dini ya Kiislamu nchini humo.
2013 Dec 01 , 08:52
Nchi tofauti mbalimbali zimepongeza makubaliano yaliyofikiwa hivi karibuni kati ya Iran na madola 6 yenye nguvu duniani kuhusiana na shughuli zake za nishati ya nyuklia. Pakistan imekaribisha makubaliano hayo ambapo Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo imesema, Pakistan ikiwa nchi ndugu na jirani na Iran siku zote imekuwa ikisisitiza umuhimu wa kadhia hiyo kutafutiwa suluhusho la amani. Uturuki pia imekaribisha makubaliano hayo ya nyuklia kati ya Iran na kundi la 5+1 na Rais Abdallah Gul wa nchi
2013 Nov 26 , 11:26
Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amebainisha sifa na hila za kidanganyifu na kutokubali haki ubeberu wa dunia unaoongozwa na Marekani na kuongeza kuwa, njia pekee ya kuweza kumkatisha tamaa adui ni kusimama kidete na kuimarisha nguvu za taifa. Aliyasema hayo Jumatano asubuhi aliponana na makumi ya maelfu ya makamanda wa jeshi la Basiji na kusema kuwa, Basiji ni moja ya madhihirisho ya uthabiti, fakhari na utukufu wa mfumo wa utawala wa Kiislamu.
2013 Nov 23 , 11:36
Harakati ya Ikhwanul Muslimin nchini Misri imetoa wito wa kufanyika mazungumzo ili kumaliza mgogoro wa kisiasa ulioibuka nchini humo baada ya rais Mohammad Mursi kuondolewa madarakani mwezi Julai.
2013 Nov 17 , 11:38
Khatibu wa sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo mjini Tehran amesema kuwa, kundi la 5+1 linapasa kutumia vyema fursa iliyopo ya mazungumzo ya nyuklia na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ili kufidia makosa liliyoyafanya huko nyuma dhidi ya taifa la Iran.
2013 Nov 16 , 10:33
Jina la Mtume wa Uislamu, Muhammad (SAW) ndilo jina mashuhuri zaidi duniani.
Hayo ni kwa mujibu wa uchunguzi wa gazeti la kila siku la Uhispania la ABC ambalo limeandika kuwa watu milioni 150 kote duniani wanatumia jina 'Muhammad.'
2013 Nov 10 , 11:28
Katibu Mkuu wa chama cha al Wifaq cha Bahrain amesema kuwa Waislamu wa madhehebu ya Shia na wapinzani wa utawala wa kizazi cha Aal Khalifa wananyimwa kazi katika idara za serikali ya Manama kwa sababu za kimadhehebu na kisiasa.
2013 Nov 03 , 09:11
Kundi la watu wanaopiga vita Uislamu nchini Ufaransa limemshambulia mwanamke mmoja Muislamu aliyekuwa na vazi la hijabu na kumjeruhi vibaya.
2013 Nov 03 , 09:10
Taasisi za serikali ya Yemen zimeanza uchunguzi wa kutafuta nakala za kale na zenye thamani kubwa za Qur’ani zilizoibiwa mwezi uliopita kutoka kwenye Jumba la Makumbusho la Taifa.
2013 Nov 03 , 09:07
Ndege za kivita za Israel zimeshambulia maeneo ya kaskazini mwa Ukanda wa Gaza huko Palestina.
2013 Oct 28 , 20:19