IQNA

Misri yamhukumu tena Mursi maisha gerezani

21:25 - June 16, 2015
Habari ID: 3315286
Mahakama ya Misri leo imetoa hukumu ya mwisho dhidi ya aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Muhammad Mursi na viongozi wengine wa Harakati ya Ikhwanul Muslimeen iliyopigwa marufuku nchini humo.

Mahakama hiyo imemuhukumu kifungo cha maisha jela Mursi na Muhammad Badii, kiongozi mkuu wa Ikhwanul Muslimeen, huku viongozi wengine wandamizi wa harakati hiyo ambao ni, Muhammad al-Shatir na Muhammad al-Baltaji na Abdul-Aati wakihukumiwa adhabu ya kifo kwa kosa la kuifanyia ujasusi Harakati ya Kiislamu ya Palestina Hamas na kuvamia jela. Hii ni katika hali ambayo, mawakili wa Ikhwanul Muslimeen mapema leo walitangaza azma yao ya kuwasilisha ombi la kutaka kuchunguzwa upya hukumu ya adhabu ya kifo, iliyotolewa huko nyuma dhidi ya rais huyo wa zamani wa Misri, Muhammad Mursi. Muhammed Tosun, mmoja wa mawakili hao amesema kuwa, wanaitaka mahakama hiyo kuangalia upya hukumu hiyo kwa kuwa imetolewa bila vigezo maalumu. Hapo jana, idadi kubwa ya raia wa nchi hiyo wanaomuunga mkono rais huyo wa zamani wa Misri, walifanya maandamano katika miji kadha ya taifa hilo la kaskazini mwa Afrika wakiitaka serikali ya Rais Abdel Fattah el-Sisi kumuachilia huru shakhsia huyo.

3315092

captcha