Yusuf Sayyid Amer, mwenyekiti wa kamati hiyo amewasilisha pendekezo hilo ili lijadiliwe bungeni.
Ameongeza kuwa tafsiri mpya ya Qur’ani itakayotayarishwa itazingatia misimamo ya wastani katika Uislamu na kuwasilisha muelekeo wenye kukabiliana na misimamo mikali.
Halikadhalika amesema tafsiri hiyo italenga kujibu maswali kuhusu Hadithi ambazo makundi yenye misimamo mikali hutumia katika kutetea misimamo yao mikali ya kidini, amesema Amer.
Wazri wa Wakfu Misri Sheikh Mukhtar Gomaa ambaye alishiriki katika kikao hicho amesema kadiri muda unavyosonga mbele kuna haja ya kuwa na tafsiri mpya za Qur’ani Tukufu.
Aidha anasema kuna mkakati wa kuhakikisha kuwa mafunzo ya kidini yanapatikana kwa lugha yenye kufahamika na waliowengi katika jamii.