Ee Mwenyezi Mungu! Nipambe katika mwezi huu wa Ramadhani kwa sitara yaani (vazi) la kukuogopa, na Unisitiri katika mwezi huu kwa vazi la kukinai na kutosheka, na Unielekeze katika mwezi huu kwenye uadilifu na usawa. Na Unisalimishe katika mwezi huu na kila nikiogopacho kwa kinga yako Ewe Mhifadhi wa wenye kuogopa.