IQNA

Amnesty yalaani ukatili wa Israel

Askari wa Israel wahujumu hospitali mjini Quds

9:52 - October 30, 2015
Habari ID: 3415418
Wanajeshi wa utawala haramu wa Israel wameishambulia hospitali katika wa Quds, inaoukalia kwa mabavu, baada ya wakuu wa hospitali hiyo kukataa kutoa taarifa kuhusu Wapalestina waliotibuwa hapo.

Alhamisi wanajeshi wa utawala katili wa Israel walishambulia Hospitali ya al-Makassed mjini Quds ambapo walitumia mabavu na kuwashambulia kwa wafanyakazi wa hospitali hiyo kwa risasi za plastiki, gurunedi za moshi na mabomu ya sauti.
Wafanyakazi wa hospitali hiyo walilalamikia vikao ukatili huo wa wanajeshi wa Israel ambao walikuwa wanataka faili za wagonjwa waliojeruhiwa katika mapambano na wanajeshi wa Israel katika ardhi za Palestina zinazokaliw kwa mabavu. Kwingineko Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Amnesty International limeulaani vikali utawala  wa Kiyauni wa Israel kwa kuwaua raia Wapalestina. Katika taarifa, Amnesty imesema hakuna chochote kinachoweza kuhalalisha hatua ya Israeli kuwaua kiholela Wapalestina.
Mwezi huu wa Oktoba pekee, wanajeshi wa Israel wamewaua Wapalestina takribani 70 tokea ianze intifada au mwamko mpya  wa kupinga jina na udhalimu wa Israel katika maeneo ya Ukanda wa Ghaza na Quds Tukufu.

3409292

captcha