IQNA – Sheikh Ahmed Ahmed Nuaina, qari mashuhuri wa Misri, amechapisha kwenye ukurasa wake rasmi wa Facebook video inayoonyesha mwanamke Mmarekani akisilimu katika moja ya misikiti nchini Marekani.
IQNA – Reza Safdari, qari mashuhuri kutoka mkoa wa Sistan na Baluchestan, kusini mashariki mwa Iran, amejiunga na kundi la wanaofuzu kuingia fainali za mashindano ya kimataifa ya Qur’ani yanayofanyika nchini Qatar.
IQNA – Jumuiya ya Wanazuoni wa Kiislamu wa Lebanon imesisitiza katika taarifa yake kwamba watu wa Venezuela, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, watazima njama ya Marekani. Wameongeza kuwa mataifa huru na yenye mamlaka yao yanapaswa kusimama pamoja kukabiliana na dhulma na jinai za Marekani na kuunda ushirikiano wa kimkakati.
IQNA – Sheikh Chems-Eddine Hafiz, mlezi wa Msikiti Mkuu wa Paris, amesema mwaka 2025 ulikuwa miongoni mwa miaka migumu zaidi kwa Waislamu nchini Ufaransa, ukitawaliwa na matukio ya vurugu yaliyofikia kiwango cha “kuuawa kwa misingi ya dini.”
IQNA – Katibu Mkuu wa Hizbullah amemkumbuka Shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani kwa kusifu nafasi yake ya kipekee katika kupinga Marekani, akieleza kuwa kazi yake ilikuwa kiini cha Mhimili wa Muqawama (Mapambano).
IQNA – Naibu mkurugenzi wa kitamaduni wa Msikiti wa Jamkaran mjini Qom, Iran, amesema zaidi ya watu 16,000 wamesajiliwa kushiriki katika ibada ya Itikafu ya mwezi wa Rajab.
IQNA – Harakati ya mapambano ya Kiislamu ya Lebanon, Hizbullah, imelaani uvamizi wa Marekani dhidi ya Venezuela na mashambulizi ya miundombinu muhimu, maeneo ya kiraia na makazi katika taifa hilo la Amerika ya Kusini.
IQNA – Sheikh Ahmed Ahmed Nuaina, qari mashuhuri kutoka Misri, alisoma Qur’an katika msikiti wa Milwaukee, jimbo la Wisconsin, Marekani, Jumamosi jioni.
IQNA-Wanaharakati wa kutetea haki za Wapalestina wamemsifu Meya wa Jiji la New York, Zohran Mamdani, kwa kufuta amri za kiutawala zilizokuwa zikizuia shughuli za makundi yanayounga mkono Palestina.
IQNA – Harakati ya Ansarullah ya Yemen imetoa tamko kali kulaani shambulio la kijeshi lililofanywa na Marekani dhidi ya Venezuela, ikilitaja kuwa kitendo cha jinai.
IQNA – Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kwamba kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu na kusimama pamoja na wananchi “Inshaallah, tutampigisha magoti adui.”
IQNA – Imam Ali (AS) si mfano tu wa uchaji Mungu kama mtu binafsi na usafi wa moyo, bali pia ni kielelezo adimu cha uongozi wa haki, uwajibikaji na unaomweka mwanadamu katikati ya utawala, afisa mmoja wa Iraq amesema.