IQNA

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran

Mataifa ya Kiislamu yawe macho kuhusu njama za maadui

0:54 - October 01, 2016
Habari ID: 3470588
Khatibu wa Swala ya Ijumaa iliyoswaliwamjini Tehran ameyaasa na kuyataka mataifa ya Kiislamu kuwa macho na njama za maadui dhidi yao.

Ayatullah Muhammad Imami Kashani amesema hayo leo mbele ya hadhara kubwa ya waumini waliohudhuria ibada ya Swala ya Ijumaa mjini Tehran na kubainisha kwamba, ulimwengu wa Kiislamu hii leo unakabiliwana njama mbalimbali za baadhi ya madola ya Magharibi na ya Kiarabu yanayoyaunga mkono makundi ya kigaidi na kitakfiri ikiwemo Saudi Arabia na kusisitiza kwamba, mataifa ya Kiislamu hayapaswi kusalimu amri mbele ya njama hizo.

Ayatullah Kashani amebainisha katika hotuba zake kwenye Swala ya Ijumaa mjini Tehran kwamba, mataifa ya Kiislamu yanapaswa kutafuta ufumbuzi wa njama zinazokabiliwa nayo katika misingi ya fikihi.

Khatibu wa Swala ya Ijumaa ameyahutubu mataifa ya Kiislamu na Kiarabu na kuyatahadharisha akiyaambia kwamba, Saudia kwa kuyaunga mkono makundi ya kigaidi na kitakfiri inafanya njama za kusukuma mbeke gurudumu la matakwa haramu ya utawala wa Kizayuni wa Israel na Marekani katika eneo la Mashariki ya Kati.

Ayatullah Kashani ametoa pongezi zake kwa welewa wa vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu katika kipindi cha Kujihami Kutakatifu kwenye vita vya kichokozi vilivyoanzisha na utawala wa dikteta Saddam dhidi ya taifa hili na kusema kuwa, vikosi hivi vimekuwa vikifanya harakati katika fremu ya kulinda thamani za mapinduzi haya ya Kiislamu na usalama wa jamii.

3534171/

captcha