Katika taarifa Wizara ya Ulinzi ya Russia, imesema, mnamo
Mei 28, ndege za kivita za Russia za Su-34 na Su-35 zilitekeleza mashambulizi
karibu na ngome ya ISIS mjini Raqqa kaskazini mwa Syria.
Taarifa zinasema
zinasema miongoni mwa waliokuwa katika mkutano wa makamanda wa ISIS walilolengwa
ni kinara wa ISIS al-Baghdadi.
Aidha mkutano huo ulikuwa na magaidi 300 ambao walikuwa na jukumu la kuwalinda makamanda hao wa ISIS aliokadiriwa kuwa 40 akiwemo al Baghdadi.
Taarifa hiyo imesema: "Kwa mujibu wa ripoti kadhaa, kiongozi wa ISIS Ibrahim Abu Bakr al-Baghdadi, ambaye aliuwawa katika hujuma hiyo ya ndege, alikuwa katika mkutano huo.