IQNA

Magaidi waua watu 30 katika hujuma dhidi ya Msikiti wa Mashia Afghanistan

9:52 - August 02, 2017
Habari ID: 3471098
TEHRAN (IQNA)-Magaidi wametekelza hujuma dhidi ya Msikiti wa Waislamu wa amdhehebu ya Shia huko Herat, Afghanistan na kuuawa waumini 30 waliokuwa katika Sala ya Ishaa Jumanne usiku.

Msemaji wa Polisi mjini Herat Abdulhai Walizada amesema kulikuwa na washambuliaji wawili ambapo mmoja aliyekuwa amejifunga mshipi wa bomu alijiripua na mweingine aliwarushia waumini gurunedi huku akifyatua risasi kiholela.

Hakuna kundi lolote lililodai kuhusika na hujuma hiyo huku wanamgambo wa Taliban ambao hutekeleza mashambulizi ya kigaidi wakisisitza kuwa halijahusika.

Rais Ashraf Ghani wa Afghanistan, ambaye serikali yake imekuwa chini ya mashinikizo kutokana na kuzorota usalama nchini humo, amelaani hujuma hiyo na kutoa wito kwa maulamaa wa Kiislamu kuzungumza wazi dhidi ya hujuma kama hizo za kigaidi.

Magaidi wa kundi la ISIS wamejipenyeza Afghanistan na katika miezi ya hivi karibuni wamehusika katika hujuma dhidi ya Waislamu wa madhehebu ya Shia ambao wengi wao ni wa kabila Hazara la waliowachache nchini humo.

Zaidi ya raia 1,700 wameuawa katika hujuma za kigaidi Afghanistan mwaka huu pamoja na kuwepo vikosi vya kigeni vinavyoongozwa na Marekani nchini humo.

3463539

captcha