Kwa mujibu wa taarifa waumini walianza kuingia misikitini Jumamosi alfajiri kwa kuzingatia kanuni za kiafia ikiwa ni pamoja na kuvaa barakoa au maski, visafishi au sanitiza na kuzingatia umbali wa mita 1.5 wakati wa Swala.
Ujerumani imeanza kupunguza zuio la kutoka nje ambalo lilikuwa linatekelezwa nchini humo kuzuia kuenea corona.
Serikali ya Ujerumani imeruhusu shule, misikiti, makanisa na viwanja vya michezo kufunguliwa hatua kwa hatua kwa sharti la kuzingatia kanuni za afya za kukabiliana na COVID-19.
Hadi sasa Ujerumani imeripoti kesi 170,000 za maambukizi ya COVID-19 ambapo watu 7,500 wamepoteza maisha kutokana na ugonjwa huo hadi kufikia Mei 10.