Katika mabadiliko hayo, Trudeau amemteua Omar Alghabra kuwa waziri mpya wa uchukuzi baada ya Navdeep Bains kustaafu.
Alghabra mwenye asili ya Saudia alichaguliwa kama mbunge mwaka 2015 na ana shahidi ya uzamili katika Uhandisi wa Mekaniki na pia ni mwanaharakati wa kijamii.
Tayari Waislamu wengine wawili wanahudumu katika baraza la mawaziri la Canada ambao ni Ahmad Hussein mwenye asili ya Somalia ambaye ni Waziri wa Familia na Ustawi wa Kijamii na Maryam Monsef mwenye asili ya Afghanistan ambaye ni Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa.