IQNA

Nasrallah: Muungano wa kijeshi wa Marekani, NATO, umeshindwa vibaya Afghanistan

10:57 - August 18, 2021
Habari ID: 3474201
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi wa harakati ya Lebanon Hezbullah anasema kushindwa kwa Marekani nchini Afghanistan kunaonyesha ujinga wa wa wakuu wa Washington na kukosekana mahesabu katika sera zao kigeni.

Sayyed Hassan Nasrallah ameyasema hayo Jumanne, katika mkesha siku ya tisa ya maombolezo ya Muharram.

Nasrallah alisema "mandhari ya Kabul inafanana kabisa na mandhari ya Saigon huko Vietnam," na kwamba "Marekani bado ina sera za kijinga katika eneo hilo, na inarudia makosa yale yale."

Kiongozi wa Hezbullah amesisitiza kwamba Rais wa Marekani Joe Biden aliondoa majeshi yake kutoka Afghanistan "kwa sababu hangeweza tena kumudu" matokeo ya kubakia katika nchi hiyo.

Kiongozi wa Hizbullah amesema kuwa, "Biden alisema kuwa alitumia zaidi ya dola trilioni na sasa Wamarekani wameondoka wakiwa wamedhalilika na wameshindwaa," na kuongeza kuwa, "Biden alitaka vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Afghanistan kupitia vita kati ya vikosi vya Taliban na Afghanistan. "

Nasrallah alisema vikosi vya muungano wa kijeshi NATO vikiongozwa na Marekani nchini Afghanistan "vilishindwa vibaya," na kwamba kujiondoa kwa fedheha kwa Marekani katika nchi hiyo kunonyesha kuwa Washington "haitapigana kwa niaba ya washirika wake."

Uvamizi ulioongozwa na Marekani dhidi  Afghanistan kwa kisingizio cha kile kinachoitwa vita dhidi ya ugaidi uliwaondoa Taliban kutoka madarakani miaka 20 iliyopita, lakini hujuma hiyo ya kijeshi ilivuruga zaidi usalama nchini humo.

Kundi laTaliban hivi karibuni lilichukua haraka udhibiti  miji mikubwa Afghanistan baada ya Biden kuamuru kuondolewa mara moja vikosi vya Marekani nchini humo.

Wanamgambo wa Taliban walizingira mji mkuu Kabul siku ya Jumapili, na kumlazimisha rais wa Afghanistan, Ashraf Ghani, kukimbia nchi hiyo. Ghani, ambaye sasa hajulikani alipo, aliondoka Afghanistan wakati Taliban iliingia Kabul bila kupingwa.

Matukio hayo yalisababisha machafuko, na maelfu ya raia wa Afghanistan na wanadiplomasia wameondoka nchini humo.

3475522

captcha