IQNA

Wapalestina 25,000 washiriki Sala ya Ijumaa Msikiti wa Al Aqsa

17:08 - January 28, 2022
Habari ID: 3474860
TEHRAN (IQNA)- Wapalestina wasiopungua 25,000 wamestahamili baridi kali na kushiriki katika Sala ya Ijumaa wiki hii katika Msikiti wa Al Aqsa ulio katika mji wa Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Palestina, pamoja na kuwa wakuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel walikuwa wameweka sheria kali za kuwazuia Wapalestina, lakini maelfu walifanikiwa kufika katika msikiti huo mtakatifu kwa ajili ya Sala ya Ijumaa.

Idara ya Wakfu wa Kiislamu Quds imetangaza kuwa Wapalestina wameshiriki katika Sala ya Ijumaa wiki hii.

Wiki hii mji wa Quds umeshudia baridi kali ambapo maeneo yote ya msikiti huo yalikuwa yamejaa theluji jambo ambalo liliwaletea furaha tele Wapalestina katika mji huo.

Children build a snowman in front of the Dome of the Rock,

Wapalestina wakifurahia theluji katika pembizoni mwa Qubbat aṣ-Ṣakhra karibu la Msikiti wa Al Aqsa katika mji wa Quds

Askari wa utawala wa Kizayuni wa Israel huwazuia Wapalestina wengi kufika katika Msikiti wa Al Aqsa wakati wa Sala ya Ijumaa.

Msikiti wa Al Aqsa umegeuzwa kuwa eneo la kutamba na kujifaragua askari wa utawala haramu wa Israel na walowezi wa Kizayuni wanaochukua hatua zinazolenga kuubadilisha utambulisho wa Kiislamu na Kikristo wa mji wa Quds (Jerusalem) na badala yake kuufanya kuwa na nembo za Uzayuni.

Utawala wa Kizayuni unachukua hatua hizo za kibeberu kuhusiana na mji wa Baitul Muqaddas na msikiti wa Al Aqsa wakati Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO lilipitisha azimio mwaka 2016 lililopinga kuwepo uhusiano wowote wa kihistoria, kidini au kiutamaduni kati ya Mayahudi na maeneo matakatifu ya mji wa Quds na hasa msikiti wa Al Aqsa na kusisitiza kuwa, msikiti huo ni mahala patakatifu kwa Waislamu.

Mji wa Quds ulipo msikiti wa Al Aqsa ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu ni sehemu isiyotenganika na ardhi ya Palestina na moja ya maeneo matatu muhimu zaidi matakatifu ya Kiislamu.

4031970

captcha