IQNA

Mashindano ya 45 ya Kitaifa ya Qur'ani ya Iran kufanyika Juni

17:32 - April 11, 2022
Habari ID: 3475111
TEHRAN (IQNA)- Raundi ya kwanza ya Mashindano ya 45 ya Kitaifa ya Qur'ani Tukufu ya Iran imepengwa kufanyika katika miezi ya Juni na Julai.

Akizungumza na IQNA, Hamid Majidimehr, Mkuu wa Masuala ya Qur'ani katika Shirika la Wakfu na Masuala ya Kheri Iran amesema usajili wa washiriki utaanza baada ya wiki mbili na kuendelea kwa muda wa mwezi moja.

Amesema raundi za michujo zitafanyika katika miji midogo kabla ya kufika katika ngazi ya mikoa  na hatimaye ngai za kitaifa.

Mashindano ya Kitaifa ya Kusoma na Kuhifadhi Qur'ani Iran hufanyika kila mwaka chini ya usimamizi wa katika Shirika la Wakfu na Masuala ya Kheri Iran.

Mashindano hayo hulenga kugundia na kukuza vipawa vya Qur'ani nchini sambamba na kuwateua wawakilishi wa Iran katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani katika maeneo mbali mbali duniani.

4046748

captcha