IQNA

Waziri Mkuu wa Malaysia

Mwezi wa Ramadhani wakati bora kwa Waislamu kuifahamu Qur'ani

17:40 - April 19, 2022
Habari ID: 3475142
TEHRAN (IQNA)- Waziri Mkuu wa Malaysia aliwataka Waislamu kuisoma na kuielewa kwa kina Qur'ani Tukufu ili wawe miongoni mwa wachamungu.

Katika chapisho kupitia Facebook mnamo Jumatatu (Aprili 18) usiku, Ismail Sabri Yaakob alisema mwezi mtukufu wa Ramadhani ni moja ya nyakati bora kwa Waislamu kuelewa yaliyomo katika Kitabu Kitakatifu ili waweze  kuishi maisha bora ya mja wa Mwenyezi Mungu.

Amesema Mtume Muhammad SAW aliteremshiwa Qur'ani Tukufu katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Aidha amesema 'Alhamdulillah, kipindi cha janga la corona kimetupatia fursa ya kusoma zaidi aya za Qur'ani Tukufu'.

Chapisho hilo la Facebook pia liliambatanishwa na bango la salamu za Nuzul Al-Quran kutoka kwa waziri mkuu.

Nuzul al-Quran inahusu tukio ambapo aya ya kwanza ya Quran iliteremshwa kwa Mtume Muhammad (SAW) katika pango la Hira.

3478553

captcha