IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Iran yatahadharisha kuhusu kushadidi chuki dhidi ya Uislamu duniani

18:08 - June 21, 2022
Habari ID: 3475406
TEHRAN (IQNA)- Balozi wa mwakilishi wa kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa ametoa indhari kuhusu kuongezeka vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu katika pembe mbalimbali za dunia.

Majid Takht-Ravanchi alitoa tahadhari hiyo jana Jumatatu katika mkutano uliofanyika kwa mnasaba wa Siku ya Kimataifa ya Kupambana na Matamshi ya Chuki.

Amesema kuongezeka wimbi la watu wa kuchocheana kwa misingi ya dini na imani za kiroho ni changamoto kubwa inayotishia jamii na mataifa mbalimbali kuishi kwa utangamano na kuvumiliana.

Mwanadiplomasia huyo wa ngazi ya juu wa Iran ameashiria ongezeko la kesi za Islamophobia duniani na kusisitiza kuwa, ni jambo la kusikitisha kushuhudia matukio ya kupigwa marufuku vazi la Hijabu katika baadhi ya maeneo na nchi, kuchomwa moto nakala za Qurani Tukufu, na kuvunjiwa heshima nembo na maeneo matukufu ya Waislamu mkabala wa kimya cha jamii ya kimataifa.

Amesema serikali zinapaswa kuhakikisha kuwa mataifa yao yanafungamana na Sura ya 20 (2) ya Mkataba wa Kimataifa Juu ya Haki za Kijamii na Kisiasa, inayompa kila mtu uhuru wa kuabudu, na kwamba ni kinyume cha sheria wao kubaguliwa kwa misingi ya dini na imani zao.

Haya yanajiri siku chache baada ya Muungano wa Kimataifa wa Wanazuoni wa Kiislamu (IUMS) kutoa mwito wa kupasishwa sheria ya kujinaisha na kupiga marufuku kuvunjiwa heshima matukufu ya dini mbalimbali kote duniani.

Hii ni katika ambayo, mataifa ya Kiislamu yanaendelea kulaani kitendo cha wanasiasa wa chama tawala nchini India cha kumvunjia heshima Mtume Muhammad SAW na matukufu ya Kiislamu.

3479395

captcha