Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar katika ujumbe huu, huku kikilaani mlipuko huo, kilisema: "Kuwashambulia waumini ndani ya Nyumba ya Mwenyezi Mungu ni ugaidi wa kumwaga damu na uko mbali na maadili ya kidini na ya kibinadamu."
Katika ujumbe huu, Al Azhar imesisitiza kuhusu kuratibiwa juhudi za nchi za Kiislamu na jumuiya ya kimataifa kukabiliana na ugaidi na kuutokomeza kabisa.
Katika muendelezo wa ujumbe wake Al-Azhar sambamba na kutoa salamu zake za rambirambi na masikitiko makubwa kwa wananchi wa Afghanistan na familia za wahanga, amemuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwasamehe na kuwarehemu wahanga wa tukio hilo la kuhuzunisha na kupona haraka waliojeruhiwa. Al Azhar imeelezea matumaini kwamba usalama na amani vitarejea Afghanistan na Waafghani kuwa salama kutokana na madhara ya ugaidi.
Ikumbukwe kwamba siku ya Ijumaa, mlipuko mbaya ulitokea katika Msikiti wa Ghazergah huko Herat, Afghanistan, na kusababisha makumi ya watu kuuawa na kujeruhiwa.
Mlipuko huu ulitokea wakati wa mkutano wa kiuchumi uliofanyika huko Herat ambao Mullah Baradar, Naibu Waziri Mkuu wa Taliban alikuwa anahudhuria kikao hicho.
4083305