IQNA

Harakati za Qur'ani

Wahifadhi 1001 wa Qur’ani Tukufu waenziwa huko Erzurum ya Uturuki

20:48 - January 14, 2023
Habari ID: 3476403
TEHRAN (IQNA) - Hafla ilifanyika Erzurum, mashariki mwa Uturuki, kupongeza mafanikio ya watu wengi ambao wameweza kuhifadhi au kujifunza Qur'ani Tukufu kwa moyo.

Kituo cha Dar al-Ifta cha Erzurum kiliandaa hafla hiyo, ambapo wahifadhi 1001 wa Qur'ani Tukufu walienziwa na kupongezwa kwa mafanikio yao makubwa.

Baadhi ya viongozi na shakhsia wa kidini na wa Qur'ani walishiriki katika mahafali hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa michezo.

Fateh Kuret, mkurugenzi wa Idara ya Masuala ya Kidini Uturuki (Diyanet) katika hotuba yake alisisitiza umuhimu wa kuhifadhi Qur'ani na kusema watu wa Uturuki wanaipenda Qur’ani na wanaitumikia.

Aidha amebainisha kuwa takriban watu 12,500 waliweza kuhifadhi Qur'ani Tukufu nchini humo mwaka jana, ambayo ni rekodi kubwa tangu kuasisiwa kwa Jamhuri ya Uturuki.

Wahifadhi wa Qur'ani wavulana na wasichana walipokea vyeti na zawadi kutokana na mafanikio hayo.

Qur’ani Tukufu ndio maandiko pekee ya kidini ambayo yamehifadhi kikamilifu na wafuasi wake.

Watu wasiohesabika katika kila umma wa Kiislamu wamehifadhi Qur’ani tangu siku ya kwanza ilipoteremshwa.

Quran ina Juzuu (sehemu) 30, Sura 114 (sura) na aya 6,236.

4114433

captcha