IQNA

Kituo cha Kimataifa cha Astronomia

Idul Fitr inatabiriwa kuwa Jumamosi katika aghalabu ya nchi

15:27 - April 17, 2023
Habari ID: 3476880
TEHRAN (IQNA) – Kituo cha Kimataifa cha Astronomia (IAC) kimesema Siku Kuu ya Idul Fitr, ambayo inaadhimisha mwisho wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, huenda ikaangukia Jumamosi.

Hakuna uwezekano wa kuona hilali ya Shawwal siku ya Alhamisi, Ramadhani 29, inayolingana na Aprili 20, na kwa hivyo Idul Fitr inaweza kuwa Jumamosi, Aprili 22, ilisema.

Shirika hilo la unajimu lenye makao yake makuu Abu Dhabi lilisema katika taarifa kwenye akaunti yake ya Twitter kwamba utabiri wake unatokana na taarifa za unajimu na kwamba tarehe kamili ya Idul Fitr itathibitishwa tu na mamlaka zinazohusika kulingana na muandamo wa mwezi mpya.

Kuonekana kwa hilali siku ya Alhamisi jioni ni ngumu sana katika aghalabu ya nchi kwani kunahitaji darubini sahihi, mwangalizi wa kitaalamu, na hali ya kipekee ya hali ya hewa. "Kuona hilaliAlhamisi ijayo haiwezekani kwa macho kutoka popote katika ulimwengu wa Kiarabu na Kiislamu. Kuona hilali siku ya Alhamisi haiwezekani kwa darubini katika nchi nyingi za Kiarabu, isipokuwa sehemu za Afrika Magharibi kuanzia Libya, na kwa hivyo Jumamosi itakuwa siku ya kwanza ya Siku Kuu ya Idul Fitr," ilisema taarifa hiyo.

4134750

Kishikizo: hilali idul fitr
captcha