IQNA

Mawaidha

Utunzaji mazingira kwa mtazamo wa Uislamu

23:38 - May 07, 2023
Habari ID: 3476968
TEHRAN (IQNA) – Mazingira ni mojawapo ya baraka kubwa zaidi za Mwenyezi Mungu, hata hivyo, wanadamu katika miaka ya hivi karibuni wameshindwa kutunza baraka hii, na wamesababisha madhara kwa neema hii.

Suala la uharibifu wa mazingira limekuwepo katika historia, hata hivyo, tatizo jipya limeibuliwa katika miongo ya karibuni nalo ni uharibu mkubwa wa mazingira. Kwa vile sayansi imeongeza uwezo wa mwanadamu kutawala maumbile na mazingira, vivyo hivyo, imeongeza uwezo wetu wa kuharibu mazingira. Katika Quran Tukufu, Mwenyezi Mungu Mtukufu anatahadharisha dhidi ya ufisadi duniani huku pia akizingatia kuhifadhi maisha.

Katika aya ya 87 ya Surah Al-Maida, tunasoma: " Enyi mlio amini! Msiharimishe vizuri alivyo kuhalalishieni Mwenyezi Mungu, wala msikiuke mipaka. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi wakiukao mipaka." Vile vile tunasoma katika aya ya 27 ya Sura Al-Baqarah: "… na wakafanya uharibifu katika nchi; hao ndio wenye khasara.."

Neema anazopewa mwanadamu duniani ni halali na zinajuzu maadamu hazisababishi uharibifu; “Kuleni na kunyweni katika vile alivyoruzuku Mwenyezi Mungu, wala msifanye uovu katika ardhi mkiharibu,” inasomeka aya ya 69 ya Surat Al-Baqarah. Kwa hiyo, kushindwa kutunza baraka za dunia kunaweza kuharibu mazingira na kusababisha uharibifu.

Katika aya ya 205 ya Surah Al-Baqarah, uharibifu wa mazingira na wanadamu umetajwa pamoja na hii inaonyesha uhusiano kati ya wawili hao: “Na anapo tawala hufanya juhudi katika nchi kwa kufisidi humo na kuteketeza mimea na viumbe. Na Mwenyezi Mungu hapendi ufisadi.”

Ndio maana tunapaswa kutunza mazingira, kama zawadi kutoka kwa Mungu, ili baraka hii isigeuke kuwa chanzo cha huzuni kwa wanadamu.

 

Kishikizo: mazingira uislamu
captcha