IQNA

Ufaransa inaongoza katika kuwakandamiza Waislamu barani Ulaya

21:06 - May 23, 2023
Habari ID: 3477035
TEHRAN (IQNA) – Msomi Muislamu wa Austria, Farid Hafez ameitaja serikali ya Ufaransa kama nchi ya Ulaya ambayo ina mtazamo mkali zaidi kwa Waislamu Waislamu.

Hafez, ambaye asili yake ni Misri, alisema viongozi wa nchi nyingi za Ulaya katika miaka ya hivi karibuni wamepitisha sera kali dhidi ya Waislamu/
Alisema Austria ilikuwa ni nchi iliyowatendea vyema Waislamu na miongoni mwa nchi chache za Ulaya zinazowatambua Waislamu kama jumuiya ya kidini na kusimamia uhuru wao wa kidini kwa kile kinachoitwa Islamgesetz (Sheria ya Kiislamu) mwaka 2012.
Hata hivyo, alisema, tangu kansela wa zamani Sebastian Kurz aingie madarakani, viongozi wa kisiasa nchini humo walianza kuwalenga Waislamu na kupitisha sera ya kuridhisha makundi ya mrengo mkali wa kulia.
Hafez alibainisha kuwa walipiga marufuku Hijabu na kufunga misikiti mingi nchini Austria.
Pia alitaja "operesheni ya usalama" mnamo Novemba 2020 ambapo polisi walivamia nyumba za makumi ya Waislamu pamoja na misikiti na taasisi za Kiislamu, akisema lengo lilikuwa kuwakandamiza na kuwaweka kando Waislamu.
Aidha alisema kati ya nchi za Ulaya, serikali Ufaransa ina mtazamo mkali zaidi katika maingiliano yake na Waislamu.
Nchini Ujerumani pia, wahafidhina ambao wamekuwa madarakani kwa miaka 16 wamechukua hatua nyingi dhidi ya Waislamu na asasi za kiraia za Kiislamu ingawa si kwa uwazi kama ilivyo Austria.
Hafez, ambaye amesimamia utungaji wa ripoti ya mwaka kuhusu chuki dhidi ya Uislamu barani Ulaya tangu mwaka 2015, anasema tangu vyama vyenye msimamo wa wastani vilivyo madarakani barani Ulaya kuanza kupitisha sera za siasa kali za mrengo wa kulia, hali imekuwa mbaya zaidi kwa Waislamu barani humo.
Nyumba ya Hafez ilikuwa moja kati ya nyumba 60 za wanaharakati wa Kiislamu na wasomi waliovamiwa mnamo Novemba 2020 kama sehemu ya kile waziri wa mambo ya ndani wa Austria aliita "Operesheni Luxor".
Hati ya upekuzi ilidai kuwa Hafez alitaka kuangamiza Misri na Israel na kuanzisha ukhalifa wa Kiislamu duniani kote na mji mkuu wake  al-Quds.
Mbali na "kuunga mkono ugaidi", polisi walimshtaki kwa uhalifu ikiwa ni pamoja na "uadui kwa serikali" na "utakatishaji wa fedha".
Akaunti ya benki ya Hafez ilifungwa, na kumuacha hawezi kulipa mawakili au kurekebisha uharibifu uliosababishwa wakati wa uvamizi.
Walakini, mashtaka ya "ugaidi" dhidi ya msomi huyo wa Austria yalifutwa mapema 2023 baada ya maandishi ya Al Jazeera kufichua kesi hiyo ilitokana na ushahidi wa uwongo na tuhuma za uwongo.

3483669

captcha