Shirika la Vitabu Adimu na Maandishi, ambalo linajishughulisha na vitabu adimu ndilo lililowasilisha Msahafu huo nadra unaokadiriwa kuwa na thamani ya euro 85,000, sawa na dirham 336,595, kwenye banda lake.
Mohammed Asif ambaye ni mmiliki wa kampuni hiyo ameeleza kuwa kuwa kampuni hiyo inamilizi hati asili ikiwemo Misahafu zaidi ya 600 ya karne nne zilizopita.
Mwezi Agosti mwaka 2021, Sheikh Sultan Bin Mohammed Al Qasimi, Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na Mtawala wa Sharjah, alikabidhi nakala nne nadra za nakala za Qur'ani Tukufu kwa Akademia ya Qur'ani Tukufu mjini Sharjah.
Misahafu hiyo nadra ni ya kutoka kipindi cha watawala wa Iran wa silsila ya Ilkhanid katika karne ya saba Hijria Qamaria. Misahafu inanasibishwa na mwandishi hati maarufu Yaqut Al Musta'simi.
3483683