IQNA

Hali ya Waislamu India

Waislamu wa Ayodhya, India wahofia ghasia kabla ya ufunguzi wa hekalu lenye utata la Wahindu

9:56 - December 21, 2023
Habari ID: 3478068
IQNA - Baadhi ya Waislamu wanaoishi karibu na hekalu jipya la Wahindu huko Ayodhya, India, wanapanga kuzihamisha familia zao kabla ya mwezi ujao wa uzinduzi wa hekalu ambalo limejengwa katika eneo la msikiti uliokuwa maarufu uliojulikana kama Masjid Babri, wakihofia kutokea mapigano na wafanyaziara wa Kihindu.

Hekalu hilo ambalo limejengwa kwenye eneo linalozozaniwa ambapo msikiti ulibomolewa na kundi la Wahindu wenye misimamo mikali mwaka 1992, limekuwa chanzo cha mvutano na vurugu kati ya Waislamu na Wahindu (Mabaniani) kwa miongo kadhaa.

Hekalu hilo lemejengwa katika eneo ambalo inadaiwa mmoja wa miungu ya Wahindu, Ram, alizaliwa. Sasa hekalu limekengwa katika ambalo ulikuwepo Msikiti wa Babri uliojengwaa karne ya 16, na ambao ulibomolewa na Wahindu wenye itikadi kali mwaka 1992, na kusababisha ghasia nchini kote ambazo ziliua karibu watu 2,000, wengi wao wakiwa Waislamu.

Safi Mohammad, fundi cherehani mwenye umri wa miaka 38 ambaye anaishi mita chache kutoka kwa hekalu, alisema atamtuma mke wake na wanawe wawili kwa jamaa zake katika mji mwingine kabla ya sherehe ya ufunguzi wa hekalu mnamo Januari 22. Alisema bado anakumbuka machafuko ya 1992, ambapo mjomba wake aliuawa kinyama.

Kulingana na maafisa wa eneo hilo, takriban Waislamu 50,000 wanaishi karibu na hekalu hilo, ambalo linatarajiwa kuvutia wafanyaziara milioni 4.5 wa Kihindu kwa mwezi.

Hekalu hilo pia linaonekana kama ushindi wa kisiasa kwa chama tawala cha Bharatiya Janata Party (BJP), ambacho kimetetea sababu ya kujenga hekalu la Ram huko Ayodhya kwa miongo kadhaa. Waziri Mkuu Narendra Modi, ambaye ni kinara wa BJP, atazindua hekalu hilo.

Mahakama pia iliamuru kutengwa kiwanja tofauti kwa ajili ya ujenzi wa msikiti unaotarajiwa kuanza mwaka ujao, takriban maili 15 (kilomita 24) kutoka hekalu hilo.

Hata hivyo, baadhi ya Waislamu wamelalamika kwamba ardhi na mali zao zimevamiwa kinyume cha sheria na Wahindu, ambao wanatumia fursa ya kupanda kwa bei ya mali huko Ayodhya kutokana na matarajio ya kuongezeka watu wanaotembelea hekalu hilo lenye utata.

Mohd Azam Qadri, kiongozi wa Bodi ya Waqf ya Kiislamu ya Sunni alisema katika barua yake kwa mamlaka za mitaa mwezi huu kwamba baadhi ya misikiti na makaburi yamekuwa yakilengwa na wanyakuzi wa ardhi.

4189117

captcha